Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Askofu Bagonza: Ibada zitarejea Mei 31, kila muumini kuvaa barakoa
Habari Mchanganyiko

Askofu Bagonza: Ibada zitarejea Mei 31, kila muumini kuvaa barakoa

Askofu Benson Kagonza, KKKT Dayosisi ya Karagwe
Spread the love

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera, Benson Bagonza amesema, ibada zilizositishwa ili kujikinga na maambukizo ya ugonjwa unaotokana na virusi vya corona (COVID-19) zitarejea tarehe 31 Mei, 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Tarehe 26 Aprili, 2020, Askofu Bagonza alitangaza kusitisha ibada na mikusanyiko yote akieleza sababu ya kufanya hivyo ni dayosisi hiyo kuwa mpakani na nchi ambazo raia wake wanatoroka na kuingia Tanzania.

Akizungumza na MwanaHALISI ONLINE leo Jumatano tarehe 20 Mei, 2020 iliyotaka kujua ibada hizo zitarejea lini, Askofu Bagonza amesema, Ibada hizo zilisitishwa kwa kipindi cha wiki nne ili kuweka mazingira sawa.

“Tuliunda kikosi kazi kupitia maeneo mbalimbali na kazi imekamilika na tarehe 31 Mei, 2020 ibada zinarejea,” amesema Askofu Bagoza.

Akitaja baadhi ya mambo iliyobaini kikosi hicho iliyopitia makanisa yote 267 ya Dayosisi hiyo ni, “kila kanisa ziwepo Ibada mbili kila Jumapili na watu watapangwa kila kitongoji kuingia kanisani.”

Askofu Bagonza amesema, kila muumini atakayefika kanisani, atapaswa kuvaa barakoa ambapo  tayari wamenunua barakoa zaidi ya laki moja.

“Tumenunua ‘themo scaner’ kupima joto, vitakasa mikono, ndoo na kila kanisa vifaa vitakuwepo bila shida,” amesema kiongozi huyo wa kiroho.

Amesema, kikosi hiko, kimebaini baadhi ya makanisa yana madirisha madogo, hivyo wamekubaliana kuyapanua pamoja na kufanya upuliziaji, “hata kama watalamu wamesema haiui, ila tunajihakikishia tunakuwa salama zaidi.”

Askofu Bagonza amesema, “makatazo mengine yamewekwa, ibada zinakuwa fupi na washirika wanakaa kwa kuzingatia umbali ili wasibanane. Haya yote tusingeweza kuyafanya wakati watu wakiwa ndani, ndiyo maana tuliamua kusitisha ili kufanya maboresho.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!