Tuesday , 23 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mitandao ya Twitter, WhatsApp, Facebook yazimwa Burundi
Kimataifa

Mitandao ya Twitter, WhatsApp, Facebook yazimwa Burundi

Pierre Nkurunziza, Rais mstaafu wa Burundi
Spread the love

MITANDAO ya kijamii ya Facebook, twitter na WhatsAapp imezimwa nchini Burundi leo tarehe 20 Mei 2020, wakati wananchi wakiendelea kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa taifa hilo. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Taharuki imetawala kwa wananchi wa taifa hilo, hasa vijana ambao wamekuwa wakijuzana mazingira ya uchaguzi kupitia mitandao hiyo. Hata hivyo, Serikali ya Bujumbura haijaeleza chochote kuhusu uamuzi huo. 

Rais Pierre Nkurunziza anaratajiwa kukoma urais muda mchache baada ya mshindi kutangazwa na kuapishwa, hata hivyo anabaki na cheo kipya cha ‘mshauri wa ngazi ya juu wa uzalendo.’

Baada ya kukabidhi madaraka, Nkurunziza atapoke malipo ya Dola za Marekani 540,000 sambamba na kupangiwa makazi ya kifahari nchini humo.

Pierre Claver Kazihise, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini humo ametoa wito kwa Warundi kupiga kura kwa utulivu wakati ambapo sehemu zingine kukiripotiwa vurugu.

Upigaji kura umeanza saa 12 asubuhi kama ilivyopangwa, watu wamesimama kwenye mistari mirefu wakisubiri kupiga kura ili kumchaua rais, mbunge na diwani.

Katika miaka 58 tangu Uhuru wa taifa hilo, uchaguzi huo utakuwa na maana kubwa kama utakwisha na Nkurunziza kukabidhia madaraka kwa njia ya amani.

Nkurunziza, ambaye sehemu kubwa ya utawala wake ‘ulilaaniwa’ kutokana na matumizi ya nguvu na kutesa wapinzani wake, baada ya kuwepo madaraka yake yatakoma kwa miaka 15, sasa madaraka yake urais yatakoma.

Evariste Ndayishimiye (CNDD-FDD), anayeaminika kurithi kiti chake kutokana na mazingira mabovu yaliyoandaliwa na serikali ya Nkurunziza kwenye uchaguzi huo, anaaminika kufanya kile kilichofanywa na Nkurunziza katika utawala wake.

Kwenye kampeni zake Ndayishimiye alisema wazi kwamba, atapita njia aliyopita Nkurunziza kwenye utawala wake. Mpinzani wake mkubwa Agathon Rwasa, anaamini kwamba atashinda lakini hana imani na tume ya uchaguzi ya taifa hilo.

“Tunahitaji uchaguzi wa Amani” amesema Kazihise alipozungumza na kituo cha habari cha taifa hilo RTNB.

“Wapiga kura wanatakiwa kuondoka kwenye eneo la kupigia kura mara baada ya kupiga kura. Haitakiwi mikusanyiko karibu na vituo vya kupigia kura,” amesema Kazihise.

Serikali ya Burundi imekataa waangalizi kutoka Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa (UN), imeamua kusimamia uchaguzi wake yenyewe bila mwangalizi yeyote kutoka nje.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!