Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe, Mbatia ‘bifu’ kali
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe, Mbatia ‘bifu’ kali

Spread the love

JAMES Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi amekataa kufanya kazi na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Kutokana na hali hiyo, Mbowe amelazimika kuunda baraza jipya la mawaziri kivuli leo tarehe 3 Aprili 2020.

“Nilimuuliza (Mbatia) kama yupo tayari kufanya kazi kwani nilimweleza nataka kuufanya mabadiliko, alisema atafurahi kama nitamuacha,” amesema Mbowe.

Mbatia amekuwa akisakamwa na makada wa Chadema kwamba, anatumika kukibomoa chama hicho. Ni baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli Ikulu, jijini Dar es Salaam. Mara kadhaa Mbatia amekuwa akipinga tuhuma hizo.

Mbatia alikutana na Rais Magfuli kama ambavyo viongozi wengine wa vyama vya upinzani akiwemo Maalim Seif Sharif Hamadi, Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo na Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) walivyokutana naye.

Kwenye baraza hilo jipya, Mbowe amewaondoa wabunge wote wanaotokana na vyama vingine na kubakisha wale wa Chadema pekee huku akieleza ‘mazingira ya siasa yamebadilika.’

Akizungumzia kuwaacha wabunge wa CUF, Mbowe amesema, uamuzi huo ni baada ya Maalim Seif kuhamia ACT-Wazalendo.

Amesema, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haikuwa ikifanya kazi na Kambi ya Prof. Lipumba, hivyo kwa kuwa Maalim Seif aliondoka CUF, hakuona sababu ya kuendelea kukihusisha chama hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!