Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wastaafu wapewa semina
Habari Mchanganyiko

Wastaafu wapewa semina

Spread the love

WIZARA ya Elimu Sayansi na Teknolojia imeandaa mafunzo ya siku tano kwa watumishi wa Umma 150 wanaotarajia kustaafu katika Wizara hiyo katika mwaka wa fedha 2020/21. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akizungumza na watumishi hao wanaotokana na Wizara hiyo, Mwenyekiti wa kamati ya Mafunzo ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa niaba ya Katibu wa Utumishi wa Umma, Prof. James Mdoe alisema kuwa ipo haja ya kutoa mafunzo kwa watumishi wa Umma ya kustaafu mara tu wanapoanza kazi.

Alisema kuwa Wizara imeona ni vyema kutoa elimu kwa watumishi wa Wizara hiyo wanaotarajia kustaafu utumishi wa Umma kwa kipindi cha Mwaka wa fedha 2020/21 ili kuwajengea uwezo na kutambua kuwa kustaafu siyo mwisho wa maisha.

Prof. Mdoe alisema kuwa kabla ya Wizara kuanza kutoa semina kwa watumishi wa Umma ambao wanatarajia kustaafu wastaafu wengi walikuwa wakikumbana na matapeli na kusababisha wastaafu wengi kuwa masikini.

Alisema kwa kuona hilo na Wizara kutambua umuhimu wa watumishi wake mwaka jana iliamua kuanzisha mafunzo kwa ajili ya kuwajenga ili watakapostaafu wajue nini ambacho wataweza kukifanya wakiwa nje ya mfumo wa kuajiliwa.

Katika hatua nyingine akizungumza na watumishi wa Umma wanaotarajia kustaafu, Prof. Mdoe alisema kuwa pindi watumishi hao watakapostaafu wanatakiwa kuwa makini na matapeli ambao ufanya kila juhudi kuwashawishi kwa kutaka kuwaingiza katika miradi mbalimbali ambayo mwisho wake uwaacha masikini.

“Naomba kuwaambia nyie mnaotarajia kustaafu wa Umma kuna dhana kuwa kustaafu ni mwisho wa maisha dhana hiyo ni potofu kabisa na ijulikane kuwa kustaafu utumishi wa Umma ni kubadilisha mfumo wa kutoka katika ajira na kuanza maisha ya kufanya kazi na jamii,” alisema Prof. Mdoe.

Kwa upande wake, Kaimu Afisa mtendaji mkuu Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Luciana Hembe, alisema kuwa mafunzo ya watumishi wa Umma wanaotarajia kustaafu yanawajengea uwezo ili wanapostaafu wasiweze kujutia kustaafu kwao.

Alisema Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknologia wameanzisha mafunzo kwa watumishi wa Umma ambao wanakaribia kustaafu ili waweze kufanya maandalizi ya kustaafu na kutambua wazi kuwa wakistaafu watafanya kitu gani ambacho hakitakuwa na hasara kwao.

Dk. Kasambara Momole ambaye ni kaimu Mkuu wa shule upande wa Taaluma, utafifi na ushauri wa kitaaluma, alisema kuwa mafumzo hayo yamekuwa na tija kwa watumishi wanaostaafu.

Naye Mwalimu Dorah Chenyambuga kutoka chuo cha Uhasibu (TIA) ambaye anatoa mada kwa watumishi wa Umma wanaotarajia kustaafu alisema kuwa watumishi pindi wanapostaafu ni lazima wawe makini katika kuandaa miradi ambayo haitawasababishia umasikini hapo baadae.

Alisema mara kadhaa wastaafu wamekuwa wakikutana na misukosuko ya kupata hasara kutokana na kuanzisha miradi ambayo hawajaifanyia utafiti.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!