April 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mangula anyweshwa sumu

Philiph Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM

Spread the love

PHILIP Mangula, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, amenyweshwa sumu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa zaidi zinaeleza, Mangula aliugua ghafla mwishoni mwa Februari mwaka huu, na baadaye alipelekwa kulazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Maradhi hayo yaliibuka tarehe 28 Februari 2020, akiwa katika Ofisi Ndogo za CCM zilizoko Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam baada ya kuhudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Kamati Kuu ya chama hicho.

Kikao hicho ndicho kilichojadili taarifa ya kamati iliyomuhoji Bernard Membe ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje katika serikali ya awamu ya nne, Yusuf Makamba na Abdulrahman Kinana (Makatibu wakuu wastaafu wa CCM).

Baada ya kikao hicho, Membe alifukuzwa uanachama wa CCM ambapo Makamba alisamehewa kutokana na kuomba msamaha huku Kinana akipewa karipio kali.

Taarifa kwamba Mangula alinyweshwa sumu imethibitishwa na Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, na kwamba watu waliohusika kwenye tukio hilo mpaka sasa hawajajulikana.

Kamanda wa Kanda ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa leo tarehe 9 Machi 2020, amesema uchunguzi wa awali uliofanywa na polisi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, umebaini kwamba mwili wa Mzee Mangula ulikuwa na sumu.

Kamanda Mambosasa amesema, uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo unaendelea, na kwmaba ukimaliza taarifa itatolewa kwa umma.

error: Content is protected !!