Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Michezo Yanga watenga Mil 200 kuimaliza Simba
Michezo

Yanga watenga Mil 200 kuimaliza Simba

Afisa Uhamasishaji na Msemaji wa Yanga, Antonio Nugaz
Spread the love

WADHAMINI wa Yanga, Kampuni ya GSM wametenga kiasi cha Sh. 200 milioni kama motisha kwa wachezaji endapo watafanikiwa kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba unatarajiwa kuchezwa Machi 8, mwaka huu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza leo na waandishi wa habari, Afisa Uhamasishaji na Msemaji wa Yanga, Antonio Nugaz na kusema kuwa kiasi hicho cha pesa kimetolewa kama motisha kwa timu kuelekea mchezo huo muhimu siku ya Jumapili.

“Shilingi milioni 200 zimewekwa mezani wadhamini wetu kampuni ya GSM kama bonus kwa ajili ya mchezo wetu kama watapata alama tatu ambazo mashabiki na wapenzi wetu tunakwenda kuzichukua siku ya Jumapili,” amesema Nugaz.

Aidha msemaji huyo aliongezea kuwa wadhamini hao wanajitolea vitu vingi kwenye klabu hiyo na siku za hivi karibuni wameanza kusimamia mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji ndani ya klabu hiyo.

Hapo awali wadhamini hao walikuwa wanatoa bonus ya Sh. 10 milioni, katika kila mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi.

Mchezo huo wa Yanga dhidi ya Simba unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 11 jioni kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Yanga ndiyo watakuwa wenyeji wa mchezo huo huku wakijinadi kutoka na alama tatu.

Viingilio katika mchezo huo ni Sh. 7,000 kwa mzunguko huku Sh. 20,000 kwa VIP B na C, huku upande wa VIP A utakuwa Sh. 30,000.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

Michezo

Beti na Meridianbet mechi za leo

Spread the love IKIWA leo hii ni Jumapili tulivu kabisa, Meridianbet wanamkwambia...

error: Content is protected !!