Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Gwajima ‘asulubiwa’
Habari Mchanganyiko

Gwajima ‘asulubiwa’

Askofu Josephat Gwajima
Spread the love

TABIA ya ukabila inayojengwa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima nchini, sasa inamtafuna mwenyewe. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Viongozi wa Kikristo na Kiislam nchini, wamemtaka Askofu Gwajima kuacha cheche za ukabila anazopandikiza kupitia Kabila la Wasukuma.

Leo tarehe 2 Machi 2020, Kamati ya Kitaifa ya Amani, Maadili na Haki za Binadamu inayojenga kwa pamoja na Maaskofu na Masheikh, imemnyooshea kidole Askofu Gwajima na kumtaka kuacha tabia hiyo.

Taarifa ya viongozi hao wa dini iliyotolewa na William Mwamalanga ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo, imewataka Watanzania kupuuza ‘ujenzi’ wa ukabila unaofanya na Askofu Gwajima kwa maelezo, kwamba ubaguzi ni dhambi.

Jana tarehe 4 Machi 2020, Askofu Gwajima alihojiwa na Jeshi la Polisi kutokana na tuhuma za kuandika vipeperushi vyenye lugha ya ukabila.

Askofu Gwajima anatuhumiwa kusambaza vipeperushi na sauti kwa lugha ya kisukuma, zenye lengo la kuhamasisha watu kuunda vikundi vya kikabila vya Whatsapp vya watu 2000 nchini.

Taarifa ya jeshi hilo ilieleza kumpa onyo kali Askofu Gwajima na wote wenye mrengo wa kupandikiza ukabila nchini. Pia kamati hiyo imelipongeza Jeshi la Polisi kwa ‘kumzima’ Gwajima na harakati zake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!