Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uboreshaji daftari wapiga kura Dar, Pwani kuanza Februari 14
Habari za Siasa

Uboreshaji daftari wapiga kura Dar, Pwani kuanza Februari 14

Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC)
Spread the love

ZOEZI la uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, kuanza tarehe 14 hadi 20 Februari, mwaka huu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ratiba hiyo imetolewa na Jaji Semistocle Kaijage, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakati akizungumza katika mkutano wa wadau wa uchaguzi nchini, jana tarehe 7 Februari 2020, jijini Dar es Salaam.

Jaji Kaijage amewataka watanzania waliofikisha umri wa kupiga kura katika mikoa hiyo, kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kujiandikisha.

“Nitoe fursa hii kwa wapiga kura wapya wote ambao wana sifa wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika daftari kudumu la wapiga kura, ili wapate fursa ya kupiga kura katika chaguzi zijazo,” amehimiza Jaji Kaijage.

Dk. Wilson Charles, Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, amewataka wananchi waliohama kutoka eneo moja kwenda jingine, kwenda kuhuisha taarifa zao katika daftari hilo.

“Tuna fursa ya kuandikisha wapiga kura wapya waliotimiza au watakaotimiza umri wa miaka 18 , kurekebisha taarifa zetu kama zimekosewa kwenye kadi kuhamisha taarifa zetu kama umehamia labda umetoka mkoa au jimbo moja kwenda lingine,” amesema Dk. Charles.

Dk. Charles amesema NEC imejipanga vyema katika kuhakikisha zoezi hilo linatekelezwa kikamilifu.

Novaita Mrosso, Afisa Idara ya Uhamiaji Dar es Salaam, amewataka wadau wa uchaguzi kushirikiana na uhamiaji ili kuwafichua raia wa kigeni wanaofanya udanganyifu kwa kujiandikisha katika daftari hilo kinyume na sheria.

“Mi naomba tu mwenyekiti na wadau hawa waendelee kushirikiana na idara ya uhamiaji na vyombo vingine,  katika kubaini na kuwafichua ambao si raia. Kila mmoja ajitoe kwa namna yake, ili kuhakikisha wanaoingia kwenye daftari ni wale wanaostahili, na kwa wale waliongia kwa bahati mbaya watoe taarifa ili waondolewe kuwe na raia wa kawaida,“ amesema Mrosso.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!