Wednesday , 15 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tunakwenda kuitawala Dodoma – Chadema
Habari za Siasa

Tunakwenda kuitawala Dodoma – Chadema

Jiji la Dodoma
Spread the love

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Kati kimeeleza dhamira yake ya kuongoza Jiji la Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Lazaro Nyalandu, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati amesema, desturi ya Chadema ni kuhakikisha inaondoka sehemu ambayo viongozi wengi wa serikali walipo.

“Tutatumia mbinu zinazojulikana na zisizojulikana kuhakikisha CCM Kanda ya Kati inafutika. CCM waanze kuona ni namna gani ya kujipanga kwa muda wa miaka mitano wakiwa wapinzani na Chadema kikiwa chama tawala,” amesema.

Hata hivyo amesema, Serikali ya Awamu ya Tano ambayo yeye ameitumikia, imetawaliwa na woga amesisitiza umuhimu wa vyama vya siasa kuwa huru kufanya siasa kwa maslahi ya umma.

Nyalandu amesema, njia ya uhuru katika demokrasia ni kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi isiyoamuliwa na mteuzi wa watendaji wa tume hiyo.

“Wakati nikiwa CCM, Singisa tulikuwa na kata moja ya uchaguzi mdogo, lakini ilikuwa ngumu na wakati huo rais wangu Kikwete (Rais Jakaya Kikwete) alinipigia simu akanieleza, kniende kuongeza nguvu.

“Wapo waliotuelewa na wengine hawakutuelewa, baada ya kupiga kura CCM tulitandikwa mbali sana, nilimpigia Rais Kikwete nikamueleza kuwa tumepigwa mbali sana, naye akasema basi kubalina na matokeo, hiyo ndio siasa tunayoitaka,” amesema Nyalandu.

Pia amesema, licha ya vyombo vya dola kufanya vizuri katika kulinda usalama wa mipaka, usalama wa raia na mali zake, lakini wafanye kazi zao kwa ueledi na kuheshimu viapo vyao.

Amesema, vyombo vya usalama visijiingizwe katika siasa na wala wasifanye kazi za siasa, kwani kazi za siasa ni za wana siasa na si vinginevyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia ateua wenyeviti wa taasisi mbalimbali

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amefanya uteuzi wa viongozi...

Habari za SiasaTangulizi

Madeleka aibwaga Jamhuri kesi za kubambikiwa

Spread the loveWakili Peter Madeleka ameshinda rufaa yake namba 263 ya mwaka...

Habari za SiasaTangulizi

Sheikh Ponda ataka kura ya maoni kuamua hatma ya muungano

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa...

Habari za Siasa

Bunge lakemea utoroshwaji mifugo kuelekea Kenya

Spread the loveKamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na...

error: Content is protected !!