Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa UPDP wamjia juu msajili
Habari za Siasa

UPDP wamjia juu msajili

Fahmi Dovutwa, aliyekuwa Mwenyekiti wa UPDP
Spread the love

WANACHAMA wa Chama cha United Peoples Democratic Party (UPDP), wameitaka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, kutovibomoa vyama vya siasa vya upinzani. Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 13 Januari 2020, kutokana na maelezo kwamba chama hicho kina mgogoro wa kiuongozi, baada ya Katibu wa Chama hicho kutangaza kumvua Fahmi Dovutwa uenyekiti wa chama hicho.

Asha Chuma, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya UPDP, ameitaka ofisi hiyo kuwa msimamizi na mlezi wa vyama vya siasa, badala kutengeneza migogoro.

“Mfululizo wa matukio haya na mengine yanaonesha kuwa, mgogoro huu ndani ya chama umechagizwa na umetenegezwa na msajili wa vyama vya siasa.

“… kama ambavyo amekuwa akifanya katika vyama vingine kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka huu. Kwa mtazamo wetu, hivi sasa ameacha kutekeleza majukumu yake yaliyopo kisheria ambayo ni kulea vyama na kuanza kuvibomoa,” amesema Chuma.

Chuma amesema, uamuzi wa ofisi hiyo kutambua kikao batili kilichodai kumvua uenyekito Dovutwa, umeonesha wazi kwamba iko nyuma ya mgogoro huo.

Nassoro Lugome, Mwenyekiti wa UPDP, Mkoa wa Dar es Salaam amemtaka Katibu Mkuu wa UPDP, kushirikiana na mwemyekiti wake, Dovutwa kuitisha mkutano mkuu wa chama kwa ajili ya kujadili mustakabali wa chama hicho.

Mbwana Kibanda, Mweka Hazina wa UPDP amesema, wataendelea kumtambua Dovutwa kama mwenyekiti wa chana hicho, hadi pale mkutano mkuu utakapoamua vinginevyo.

Kibanda amesema, Katiba ya UPDP inamtambua Dovutwa kama mwenyekiti halali wa chama hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!