CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Kati kimeeleza dhamira yake ya kuongoza Jiji la Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Lazaro Nyalandu, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati amesema, desturi ya Chadema ni kuhakikisha inaondoka sehemu ambayo viongozi wengi wa serikali walipo.
“Tutatumia mbinu zinazojulikana na zisizojulikana kuhakikisha CCM Kanda ya Kati inafutika. CCM waanze kuona ni namna gani ya kujipanga kwa muda wa miaka mitano wakiwa wapinzani na Chadema kikiwa chama tawala,” amesema.
Hata hivyo amesema, Serikali ya Awamu ya Tano ambayo yeye ameitumikia, imetawaliwa na woga amesisitiza umuhimu wa vyama vya siasa kuwa huru kufanya siasa kwa maslahi ya umma.
Nyalandu amesema, njia ya uhuru katika demokrasia ni kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi isiyoamuliwa na mteuzi wa watendaji wa tume hiyo.
“Wakati nikiwa CCM, Singisa tulikuwa na kata moja ya uchaguzi mdogo, lakini ilikuwa ngumu na wakati huo rais wangu Kikwete (Rais Jakaya Kikwete) alinipigia simu akanieleza, kniende kuongeza nguvu.
“Wapo waliotuelewa na wengine hawakutuelewa, baada ya kupiga kura CCM tulitandikwa mbali sana, nilimpigia Rais Kikwete nikamueleza kuwa tumepigwa mbali sana, naye akasema basi kubalina na matokeo, hiyo ndio siasa tunayoitaka,” amesema Nyalandu.
Pia amesema, licha ya vyombo vya dola kufanya vizuri katika kulinda usalama wa mipaka, usalama wa raia na mali zake, lakini wafanye kazi zao kwa ueledi na kuheshimu viapo vyao.
Amesema, vyombo vya usalama visijiingizwe katika siasa na wala wasifanye kazi za siasa, kwani kazi za siasa ni za wana siasa na si vinginevyo.
Leave a comment