Thursday , 16 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto kusuka, kunyoa Febr 10 
Habari za Siasa

Zitto kusuka, kunyoa Febr 10 

Spread the love

UAMUZI wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kuhusu kesi ya uchochezi namba 327/2018 inayomkabili Zitto Kabwe, kwamba ana kesi ya kujibu ama la! utajulikana tarehe 10 Februali 2020. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Upande wa Jamhuri umewasilisha mashahidi 15 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambapo tayari umefunga pazia la ushahidi wao. Kwa sasa Hakimu Huruma yupo likizo.

Leo tarehe 10 Januari 2020, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Vicky Mwaikambo, wakili wa serikali mkuu Tumain Kweka, ameiambia mahakama, upande huo umemaliza kutoa ushahidi wao na wamewasilisha hoja za kuitaka mahakama kwa ushahidi huo ione kuwa Zitto, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo anakesi ya kujibu.

Wakili wa utetezi Bonifacia Mapunda, ameieleza mahakama kuwa wamejibu hoja hizo na kwamba, hawaoni sababu ya kuongeza hoja (Rejoinder).

Hakimu Mwaikombo amesema, mahakama itatoa uamuzi tarehe 10 Februari mwaka 2020. Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi anayodaiwa kuyatenda tarehe 38 Oktoba 2018.

Anadaiwa kutenda makossa hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari, uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama hicho, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia ateua wenyeviti wa taasisi mbalimbali

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amefanya uteuzi wa viongozi...

Habari za SiasaTangulizi

Madeleka aibwaga Jamhuri kesi za kubambikiwa

Spread the loveWakili Peter Madeleka ameshinda rufaa yake namba 263 ya mwaka...

Habari za SiasaTangulizi

Sheikh Ponda ataka kura ya maoni kuamua hatma ya muungano

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa...

Habari za Siasa

Bunge lakemea utoroshwaji mifugo kuelekea Kenya

Spread the loveKamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na...

error: Content is protected !!