Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Michezo Simba, Yanga mambo mazito Kombe la Shirikisho
Michezo

Simba, Yanga mambo mazito Kombe la Shirikisho

Spread the love

DROO ya hatua ya 32 na 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho (FA CUP) imechezeshwa leo ambapo vigogo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba na Yanga zitakutana na wakati mgumu baada ya kupangiwa timu ambazo zilizowasumbua kwenye Ligi Kuu licha ya kupata faida ya kuwa nyumbani. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwenye droo hiyo klabu ya Simba imepangwa kucheza na Mwadui kwenye hatua ya 32 huku Yanga ikipangwa kucheza na klabu ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya na mechi zote mbili zitapigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Ikumbukwe Mwadui FC ndio klabu pekee iliyomfunga Simba kwenye michezo ya Ligi Kuu baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye Uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Oktoba 30, 2019 na wawili hao kukutana tena kwenye kombe la FA kutafanya mchezo huo kuwa mgumu.

Kwa upande Tanzania Prisons ambayo imepoteza mchezo mmoja tu kwenye Ligi kuu waliopoteza mbele ya Yanga kwa bao 1-0 mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Samora Iringa na wawili hao watakutana tena kwenye hatua ya 32 ya michuano hii huku mchezo huo bado ukionekana bado kuwa mgumu kwa pande zote.

Fainali ya michuano hiyo kwa mwaka huu imepangwa kuchezwa mkoani Rukwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandera huku lengo likiwa kuhamasisha mchezo wa soka kwa mkoa huko kutokana na kushindwa kuwa na uwakilishi wa klabu yoyote kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Michezo mingine ya hatua hiyo ya 32 ni Namungo FC vs Biashara, Mtibwa vs Sahare All Stars, JKT Tanzania vs Tukuyu Stars, Azam FC vs Friends Rangers, Kagera Sugar vs Mighty Elephant, Lipuli FC vs Kitayosa FC, Gwambina vs Ruvu Shooting., African Sports vs Alliance, Polisi Tanzania vs Mbeya City, Ndanda SC vs Dodoma FC, Majimaji FC vs Stand United, Ihefu FC vs Gipco, KMC vs Pan African na Panama vs Mtwivila.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!