Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Meya Dar aivimbia CCM, atinga ofisini
Habari za Siasa

Meya Dar aivimbia CCM, atinga ofisini

Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam akiwa ofisini kwake kuendelea na kazi
Spread the love
LICHA ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumvua madaraka Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam (Chadema), leo tarehe 10 Januari 2020 ametinga ofisini na kuendelea na kazi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Jana tarehe 9 Januari 2020, madiwani wa CCM kupitia kikao cha Baraza la Madiwani kilichoitishwa na Sipora Liana, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, ilitangaza kumvua madaraka Isaya. Ni baada ya kushindwa kufanya hivyo kupitia sanduku la kura.

Ikiwa ni siku moja baada ya ‘kutimuliwa’ na madiwani wa CCM, Isaya amepuuza tamko hilo na kuwasili ofisi kwake huku akisema “mimi bado Meya halali wa Jiji la Dar es Salaam.”

Isaya amewaeleza wanahabari, kwamba ataendelea na majukumu yake, kwa kuwa uamuzi uliofanyika jana katika kikao cha baraza hilo, ulikuwa batili.

Na kwamba, angeacha kuendelea na majukumu yake, kila mtu angemshangaa na kumuona mjinga, kwa kuwa mchakato ulitumika kumuondoa ulikuwa kinyume na sharia.

“Nimekuja kuwatumikia wana Dar es Salaam, kwa sababu ni kipofu asie kuwa na uwezo wa kuelewa, ndio asingekuja ofisini. Kila mtu angenishangaa, huyu jamaa hawa watu hawajamuondoa madarakani, kura hazikufika na ukumbuke kama kura haijafika azimio lao linajiondoa moja kwa moja,” ameeleza.

Amesema, kwa sasa hana shtaka lolote linalomkabili labda wanaotaka kumng’oa, waanze mchakato huo mpya, baada ya njama zao za awali kugonga mwamba.

“Kwa hiyo sina tena shtaka lolote labda waanze tena upya. Kanuni inasema, labda waanze upya mchakato wa kuniondoa ofisini sababu kura kumi na saba hawakupata.

“Kanuni ya 84 inasema, wajumbe 2/3 ya wajumbe watapiga kura ya kumuondoa meya madarakani, hawakupata wajumbe wa halmashauri nzima ya Dar, walichofanya walikuwa na kura zao 16 mfukoni na hazikutosha,” amesema Meya Mwita.

Isaya amewashauri wanaotaka kumng’oa, wagome kushiriki vikao vya baraza la halmashauri hiyo mara tatu mfululizo, hapo watafanikiwa kumng’oa kwa urahisi.

“Na mimi nawaomba kuna njia tatu za kuniondoa, wakitaka kuniondoa upesi wagome kuja kwenye vikao vya mabaraza, wakigoma mara tatu baraza la jiji litakuwa limevunjwa, likivunjwa sasa hapo nitakuwa nimeondoka sababu hawanitaki mimi,” amesema Meya Mwita na kuongeza;

“Lakini kama wanasema wanaridhika na kazi, nafanya vizuri wananipenda basi tuendelee kufanya kazi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!