Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sakata la Meya Dar: Mahakama yambwaga
Habari za Siasa

Sakata la Meya Dar: Mahakama yambwaga

Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam akimsikiliza wakili wake mahakamani
Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imesema, haiwezi kuzuia ‘meya’ wa jiji hilo, Isaya Mwita kuondolewa madarakani. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Imeeleza, Mwita hakuwasilisha uthibitisho wa uwepo wa kikao cha kumuondoa madarakani, wala hasara atakayoipata endapo akiondolewa.

“Mahakama hii inatupilia mbali hoja za kutaka muombaji (Mwita) kubaki katika nafasi byake ya umeya.

“Ni kwasababu, hoja za wakili wa muombaji hazina miguu ya kusimamia kwa kushindwa, kufuata vigezo ikiwemo uwepo wa kikao cha kutaka kumtoa madarakani,” amesema Hakimu Mkazi, Janeth Mtega.

Uamuzi huo unatokana na maombi ya Isaya, aliyoyawasilisha mahakamani hapo tarehe 6 Januari 2020, ya kutaka kuzuia kikao cha Baraza la Madiwani kilichokuwa na ajenda ya kumng’oa madarakani.

Kikao hicho kiliitishwa na Sipora Liana, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, miongoni mwa ajenda za kikao alichokiitisha jana tarehe 9 Januari 2020, ni kupokea ripoti iliyoundwa na Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuchunguza tuhuma za Isaya.

Isaya anadaiwa kutotumia kiasi cha Sh. 5.8 bilioni, zilizotokana na mauzo ya hisa za Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), ambalo lilikuwa mali ya jiji.

Shirika la UDA, ambalo mwaka 1983 Msajili wa Hazina alitoa asilimia 51 ya hisa kwa Halmashauri ya Jiji, huku serikali kuu ikibakiwa na asilimia 49.

Anatuhumiwa kushindwa kuongoza kikao cha baraza la madiwani na kupendelea baadhi ya mameya kuingia katika kamati za fedha.

Pia anatuhumiwa kuwa na matumizi mabaya ya gari umma kwa kulisababishia kupata ajali, jambo ambalo meya amekuwa akijibu kwamba, yeye siyo dereva wa gari hilo.

Hakimu Mtega alisimama ghafla kusoma uamuzi kwa huo kwa dakika 13 (kuaniza saa 12:20 hadi 12:33 mchana), akisoma uamuzi huo, ametoa hoja kadhaa;-.

Amesema, muombaji alikuwa na wajibu kuthibitisha hasara atakayoipata, endapo mahakama haitatoa amri ya kusema abaki kwenye nafasi yake.

Hakimu Mtega alianza kwa kuangalia nini maana ya mtu kubaki katika nafasi yake, ambapo alitumia Kitabu cha Marekani kilichoelezea kuwa ni “vitu ama mtu kubaki katika nafasi yake kabla ya mfarakano kutokea.”

Amesema, ili kitu kibaki katika nafasi yake, inatakiwa kuwepo kwa zuio la awali ili kuwezesha hicho kitu kibaki katika nafasi yake, na kisiondoshwe na kibaki katika hali ya amani.

Akihusisha na maombi ya kesi hiyo, Hakimu Mtega amesema, mahakama hiyo ina maoni kwamba, wakili wa muombaji alikuwa na wajibu wa kuthibitisha uwepo wa kikao cha kumuondoa madarakani Isaya kwa kutoa uthibitisho.

Na kwamba, aonyeshe suala la kuondolewa kwa Isaya madarakani lipo na pia kuipa mahakama maelezo ya kumuondoa madarakani katika nafasi yake ya umeya.

“Mahakama hii imeona wakili wa muombaji ameshindwa kutoa details (maelezo ya kina) za uwepo wa kikao cha kumuondoa muombaji (Isaya Mwita) katika nafasi yake.

“Pia alitakiwa aeleze sababu za kutaka muombaji abaki kwenye nafasi yake, pia ilibidi ajiulize je, muombaji atapata hasara yoyote endapo mahakama itashindwa kutoa uamuzi? hivyo hoja hizo zilipaswa kutolewa mahakamani,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!