Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sumaye: Nina asilimia chache kupita
Habari za SiasaTangulizi

Sumaye: Nina asilimia chache kupita

Frederick Sumaye, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Pwani
Spread the love

FREDERICK Sumaye, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Pwani amewataka wagombea kwenye kanda hiyo, kutojenga chuki pale wanaposhindwa. Anaripoti Hamis Mguta, Kibaha … (endelea).

Amesema, yeye mwenyewe ni mgombea pekee kwenye nafasi ya uenyekiti wa chama hicho Kanda ya Pwani, lakini hajui kama atapigiwa kura za ndiyo.

“Inawezekana kwenye kutafuta kura, kumesemwa maneno ya hapa na pale, lakini baada ya uchaguzi naomba yawe yameisha, unapogombea kuna kupata na kukosa.

“…hata mimi ambaye ninagombea mwenyewe ambaye natetea kiti, nina asilimia chache kwasababu ninapigiwa kura,” amesema Sumaye.

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 28 Novemba 2019, katika Hoteli ya Njuweni, Kibaha mkoani Pwani wakati akifungua rasmi mkutano wa Baraza la Uongozi la Kanda hiyo.

Sumaye amewataka wagombea kuwa na uwezo wa kuhimili matokeo, na kwamba haiwezekani wote wakapata nafasi wanazozigombea.

“Lazima uwe na kifua cha kubeba kushinda na kushindwa, ukishindwa usinune nje ya mlango huu, naomba tukitoka nje wote sisi ni timu ya washindi, huwa nasema kama unajijua una presha kwamba ukikosa hauwezi kuvumilia, ni afadhali ujitoe,” amesema.

Baadhi ya wanachama katika uchaguzi huo, hawakuruhusiwa kuingia kwenye ukumbi wa uchaguzi kutokana na idadi yao kuwa kubwa.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria uchaguzi huo ni pamoja Meya wa Ubungo, Bonoface Jacob; Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es  Salaam; Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo; Ole Sosopi, Mwenyekiti wa Bavicha na wajumbe wa Kamati Kuu ya Kanda ya Pwani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

error: Content is protected !!