April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Afya ya Mbowe mgogoro, mawakili ‘wamkomalia’

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imeahirisha shauri namba 112/2019, linalowakabili viongozi tisa wa Chadema, kutokana na kutetereka kwa afya ya mshtakiwa namba moja, Freeman Mbowe. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa na wenzake wanane, wanakabiliwa na mashitaka 13, yakiwemo kufanya maandamano kinyume cha sheria na uchochezi.

Watuhumiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Dk. Vincent Mashinji, Katibu Mkuu; John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Bara na Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

Pia Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini; John Heche, Mbunge wa Terime Vijijini.

Leo tarehe 28 Novemba 2019, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ameahirisha shauri hilo mpaka kesho tarehe 29 Novemba 2019, baada ya kusikiliza hoja za upande wa utetezi waliomba hairisho kwa sababu afya ya Mbowe haijaimarika.

Awali, upande utetezi uliongozwa na Wakili Peter Kibatala na Selemani Makaka, uliionesha mahakama hiyo  vyeti vya kuruhusiwa na kupokelewa Mbowe kwenye Hospitali ya Agha Khan.

Kibatala amedai, Mbowe ametolewa Hospitali lakini hajapona na kwamba leo alikuwa na ahadi ya kuonana na daktari saa nne.

Upande wa serikali uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, Joseph Pande; Wakili wa Mwandamizi Wankyo Simon, Wakili wa Serikali, Salim Msemo na Jackline Nyantori umedai kuwa, mshtakiwa huyo alihudhuria mahakama tarehe 26 Novemba 2019, hakueleza kama hajapona wala kuweka ahadi yake na daktari.

Wakili Pande, amedai kuwa Mbowe jana alikuwa kwenye shughuli zake za kisiasa. Upande huo umeiomba mahakama kuruhusiwa kuendelea kwa shahidi wa pili ambaye ndio mshtakiwa wa pili kuendelea na utetezi.

error: Content is protected !!