Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Handeni kupanda shamba la kuni
Habari Mchanganyiko

Handeni kupanda shamba la kuni

Spread the love

SHUGHULI za utafutaji nishati ya kupikia nyumbani (kuni) kwenye misitu zinapaswa kubadilika na kutafuta kwenye shamba binafsi jambo litakalosaidia kuendeleza uhifadhi wa misitu na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Anaripoti Christina Haule, Tanga … (endelea).

Wanawake katika kijiji cha Mazingira tarafa ya Handeni jijini Tanga walisema hayo jana wakati wakizungumza na waandishi wa habari waliotembelea msitu wa talawe uliopo wilayani Handeni, Tanga, baada ya kupata mafunzo kupitia programu ya kuendekeza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu (FORVAC).

Mmoja wa wanawake hao, Mwanaidi Mkomwa, alisema wakiwa wasimamizi na wahifadhi wazuri wa msitu wamekuwa wakiona manufaa makubwa baada ya kutafuta kuni kwenye mashamba yao na sio kwenye misitu.

Alisema, ni vema wanawake wenzao wanaoishi pembezoni mwa misitu nchini wakaona haja ya kuacha tabia ya kuharibu mazingira kwa kuchanja kuni na mkaa bali watumie mashamba waliyonayo kupata nishati hiyo.

Mkomwa ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya msitu wa kijiji alisema, wakiwa wanawake wanaendelea kunufaika na msitu huo wenye kuendelea kuimarika kimazingira wanapata maji ambayo hayakauki na kuendelea kuyatumia kwani yapo muda wote.

Alisema, usimamizi shirikishi na uhifadhi wa misitu umesaidia misitu hiyo kuendelea kuwa bora na kusababisha mvua kunywesha kila mara.

Mkomwa alisema awali kabla ya program ya FORVAC watu walikatazwa kukata kuni na kuchoma mkaa lakini walitafuta nafasi wakaiba lakini baada ya programu ulinzi umeimarika na watu wameacha kukata na sasa wanatumia kuni kutoka kwenye mashamba yao kwa kutumia miti ya asili na pengine kuvuna miti mikubwa baada ya kupata kibali kutoka maliasili kwa mujibu wa sheria.

Awali Katibu wa kamati ya wasimamiaji misitu ya kijiji hicho, Mohamed Bakari alisema licha ya changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo ikiwemo ukosefu wa vifaa maalum vya kisasa vya kukabiliana na majangili ikiwemo bunduki, ukosefu wa viatu vya kutembelea msituni na ukosefu wa usafiri wa uhakika wa kuwafikisha msituni wakati wowote, wanaendelea kusimamia na kuhifadhi misitu baada ya kuanza kuona manufaa mbalimbali.

Aliyataja manufaa hayo kuwa ni pamoja na tangu waanze kuhifadhi msitu, hawajawahi kupata fedha lakini mwaka 2018 walipoanza kusimamia uhifadhi kwa maelekezo ya FORVAC, wamefanikiwa kukamata mbao haramu na kuziuza na kuwasilisha fedha kwenye uongozi wa kijiji ambapo wao walipata Sh. 600,000 kama faida baada ya makato ya kijiji kisheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!