Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko MPFCR: Vijana jiepusheni na mihadarati
Habari Mchanganyiko

MPFCR: Vijana jiepusheni na mihadarati

Waathirika wa dawa za kulevya wakishiriki uandaji wa miti Kigamboni
Spread the love

TAASISI ya Kinamama na Kinababa kwa Mageuzi ya Jamii (MPFCR), imewataka vijana kuacha matumizi ya mihadarati kutokana na madhara yake. Anaripoti Kamote Martin … (endelea).

Pia imewataka vijana hao kuacha kulalamika kukosa ajira na badala yake watumie fursa zinazowazunguka ili wajipatie kipato.  

Emmy Jahai, Mkurugenzi Mtendaji wa MPFCR ametoa kauli hiyo leo tarehe 4 Oktoba 2019, wakati wa zoezi la usafi na kupanda miti katika Kituo cha Polisi cha Kigamboni.

Amesema, vijana wengi hawajishughulishi na kazi za kuwaingizia kipato na kwamba, wanakaa vijiweni huku wakilalamika kukosa ajira.

Amesema, taasisi yake imekua ikifanya jitihada ya kuwasaidia vijana wenye uraibu wa madawa ya kulevya, ambapo baadhi yao wameacha.

“Zoezi tunalofanya leo ni kufanya usafi, kupanda miti pamoja na kutoa cheti cha heshima kwa mkuu wa kituo hiki cha polisi (ASP Said Msisiri), ikiwa ni kutambua mchango wake wa kuthamini na kujali jamii katika kupambana na vitendo vya uhalifu hapa Kigamboni,” amesema Jahai.

Awali, akisoma risala baada ya zoezi hilo, Dorah Mushi ambaye ni mratibu  wa zoezi hilo amesema, awali kulikua na maeneo mengi hatari kwa watu kutekwa mchana, lakini kwa sasa ulinzi na usalama umeimarishwa.

Ametaja maeneo hayo kuwa ni Midizini, Tungi, Minazi Mikinda, Vijibweni, Feri Bandari, Geza Ulole, Maeneo ya Beach.

ASP Msisiri amesema, Jeshi la Polisi litaendelea kupambana na baadhi ya mawakala wa madawa za kulevya.

Amesema, MPFCR inapaswa kuigwa kwa mchango wake wa kuanzisha kituo cha kuwahudumia watu wenye uraibu wa madawa ya kulevya (Sobber’s House).

Amina Mbonde, mmoja wa waathirika wa madawa ya kulevya ameshauri vijana kuacha matumizi ya dawa hizo kwa kuwa yana madhara mengi ikiwa ni pamoja na matatizo ya akili n ahata kifo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

Habari Mchanganyiko

GGML yaja na teknolojia za kisasa maonesho ya OSHA Arusha

Spread the loveKATIKA kuelimisha wananchi na washiriki wa maonesho ya usalama na...

error: Content is protected !!