Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa JPM ‘amchomea utambi’ Mbunge Chadema
Habari za Siasa

JPM ‘amchomea utambi’ Mbunge Chadema

Spread the love
RAIS John Magufuli amewambia wananchi wa Kata ya Mahenge wilayani Mbozi, Songwe kwamba angekuwa mbunge wao, asingeruhusu kuwachangishwa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Amewaambia wananchi hao kuwa “nawapenda” na kwamba, wanasiasa wanapoomba kura hutoa ahadi nzuri ambazo hawazi kutekeleza na kuwaacha na changamoto nyingi.

Rais Mgufuli ametoa kauli hiyo leo tarehe 4 Oktoba 2019, wakati akizungumza na wananchi wa kata hiyo iliyomo katika jimbo la Mbozi waliohudhuria katika mkutano wake.

Jimbo hilo linaongozwa na Paschal Haonga kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Kiongozi huyo wa nchi amewaambia wananchi hao, kwamba anawapenda hata kama wao hawampendi.

Amesema, hana uhakika kama wananchi hao wanampenda, kwa kuwa wakati wa kuchagua viongozi huwa wanabadilika.

“Nisikilizeni, si ndio maana nimesimama hapa? Au hamtaki nisimame hapa? nimesimama hapa ndugu zangu sababu nawapenda hata kama ninyi hamnipendi. Mnanipenda kweli (wananchi ndio), wangapi wananipenda?” amehoji na kuongeza;

“Mimi sina uhakika sana sababu inapofikaga wakati wa kuchagua mnabadilika, mmeshajifunza?” wananchi wakajibu ‘ndioooo’.

Hata hivyo, amewataka kuwa makini wakati wanapochagua viongozi, hasa kujihadhari na ahadi nzuri za wanasiasa ambao huzitoa licha kuwa hawazi kutekeleza.

“Mnapomaliza uchaguzi maana yake mnatupa mamlaka kwa miaka 5, kama mnapata raha ni ya miaka 5 na kama mnapata hasara ni ya miaka 5. Na nyie mnafahamu saa nyingine, sisi wanasiasa tunapokuja kuomba kura maneno tunayozungumza ni matamu.

“Na mnashangalia, sasa haya ndio kujifunza kwake. Mmesema kuna michango mingi hapa. Mnatakiwa mchangie kiasi gani hapa. Unajua watu wa kuulizwa michango ni wabunge wenu na madiwani wenu,” amesema Rais Magufuli na kuongeza:

“Kama diwani alikula hela, apelekwe mahakamani. Kama viongozi wengine hawakufuatilia hili. Ningekua mbunge nisingekubali wananchi wangu wachangishwe na kama ningekuwa diwani ningefanya hivyo. Naomba nichangie mil 5 hapa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!