Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanaharakati wapinga picha za watuhumiwa wa ukahaba kusambazwa
Habari Mchanganyiko

Wanaharakati wapinga picha za watuhumiwa wa ukahaba kusambazwa

Spread the love

MTANDAO wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia (MKUKI) umelaani kitendo cha wanawake wanne wanaotuhumiwa kwa kosa la ukahaba, kudhalilishwa mitandaoni. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Picha za wanawake hao akiwemo Shania Hamada, Najia Alfani, Amina Mawazo zinazoonesha wakibeba mabango yenye makosa yao na mahali walipotenda, zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii, tangu jana tarehe 25 Julai 2019.

Wakili Anna Henga, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC) akisoma tamko la MKUKI leo tarehe 26 Julai 2019, amesema mtandao huo pamoja na wanaharakati wengine wanapinga kitendo hicho, kwa kuwa ni  ukiukwaji wa haki za binadamu.

Wakili Henga ameeleza kuwa, kitendo hicho ni udhalilishaji wa utu wa mwanamke pamoja na kuingilia uhuru wao wa faragha.

Amesema picha hizo zilipigwa na maofisa wa polisi katika Kituo cha Polisi cha Murahati, na kwamba walizungumza na mkuu wa kituo hicho ambaye alithibitisha zilipigwa kituoni hapo kwa manufaa ya kazi, na si kusambazwa kama ilivyotokea.

Kufuatia hatua hiyo, MKUKI ameliomba Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua za kinidhamu waliohusika kusambaza picha za wanawake hao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!