Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli azindua Stigler’s Gorge, aisitiza ushiriki wa JKT
Habari za Siasa

Rais Magufuli azindua Stigler’s Gorge, aisitiza ushiriki wa JKT

Spread the love

RAIS John Magufuli leo tarehe 26 Julai 2019 amezindua ujenzi wa Mradi wa Uzalishaji Umeme katika Mto Rufiji ‘Stigler’s Gorge, unaogharimu kiasi cha Sh. 6.5 Trilioni unaotarajiwa kumalizika tarehe 13 Julai 2022. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Rais Magufuli ameshauri askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kushiriki katika ujenzi huo, ili wapate ujuzi watakaoutumia katika ujenzi wa miradi mingine.

“Vyombo vya ulinzi na usalama vichukue mradi huu kama mbinu ya serikali, nitashangaa kuona JKT hawahusiki katika kufanya mradi huu. Ili kusudi utalaamu watakaoupata wautumie kujenga miradi mingine,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameagiza mamlaka husika kushughulikia haraka vibali vya wafanyakazi wa kigeni, ili ujenzi huo uanze haraka. Pia ameagiza Wizara ya Nishati kuhakikisha kwamba mradi huo unatumia bima ya serikali kwa asilimia 100.

“Suala la vibali vya wafanyakazi lishughulikiwe mapema, mnachukua muda mrefu kwa ajili ya vibali wanavyokuja kutekeleza mradi huu. Pamekuwa na mabishano kati ya kampuni inayojenga na kampuni ya bima, natoa maelekezo, bima ya mradi huu asilimia 100 lazima itolewe na bima ya serikali,” ameagiza Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Rais Magufuli ameagiza wananchi wanaoishi karibu na eneo la mradi kupewa kipaumbele cha ajira, huku akitoa wito kwa watakao bahatika kupata kazi kuwa waaminifu.

Rais Magufuli ameagiza Kamati za Ulinzi na Usalama katika Mkoa wa Pwani na Morogoro kushirikiana kwa pamoja kulinda rasilimali za ujenzi wa mradi huo.

“Mtakaofanikiwa kupata mradi huu, msiibe vifaa. Kwanza kuiba ni dhambi lakini pia mtakua mnaiibia serikali na kujiibia wewe mwenyewe na kuchelewesha mradi,” amesema Rais Magufuli.

Kuhusu mradi wa Stiglers’s Gorge, Rais Magufuli amesema utachochea maendeleo ya kiuchumi,  ikiwemo kuimarisha hali ya upatikanaji umeme, kuchochea shughuli za uvuvi, kilimo na utalii.

Rais Magufuli amesema mradi wa Stigler’s Gorge utahifadhi mazingira ikiwemo kupunguza shughuli za ukataji miti kwa ajili ya kupata mikaa na kuni, kwa kuwa mradi huo ukikamilika umeme wa uhakika utakuwepo na wa gharama nafuu kwa matumizi ya majumbani.

Dk. Medard Kalemani, Waziri wa Nishati amesema mradi huo unagharimu kiasi cha Sh. 6.5 Trilioni na kwamba serikali imetoa asilimia 15 ya fedha hizo.

“Mradi utatekelezwa kwa miezi 42, mpaka sasa miezi 6 imekwisha imebaki 36, tarehe 13  Juni 2022 kwa hali inavyoendelea mradi utakuwa umekamilika na kukabidhiwa kwa Watanzania,” amesema Dk. Kalemani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

error: Content is protected !!