Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Siyo Asasi zote zinafanya vibaya
Habari Mchanganyiko

Siyo Asasi zote zinafanya vibaya

Spread the love

MKURUGENZI wa asasi isiyokuwa ya kiraia ya Women Wake Up (WOWAP), Fatuma Tawfiq, amesema kuwa siyo kweli kuwa asasi za kiraia hazifanyi kazi yake kwa jinsi isivyotakiwa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Tawfiq ambaye ni Mbunge wa Viti maalumu ametoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa akifungua mkutano ulioandaliwa na asasi isiyokuwa ya kiraia ya Foundation For Civil Society kwa kuwashirikisha waandishi wa habari wa mkoa wa Dodoma pamoja na asasi za kiraia juu ya mashirikiano katika kazi za kila siku.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo alisema kuwa kumekuwepo kwa tuhuma kuwa asasi za kiraia  azifanyi kazi yake kama inavyotakiwa.

Amesema asasi za kiraia zinafanya kazi kulingana na malengo ambayo yamekusudiwa na zimekuwa zikitumia fedha kwa lengo la kusaidia jamii na si vinginevyo.

“Nataka niwaambie kuwa asasi za kiraia zimekuwa zikifanya kazi yake kwa malengo yaliyokusudiwa na zimekuwa zikitumia fedha kwa makusudi ya kufikia jamii.

“Hivyo siyo kweli kuwa asasi za kiraia zinatumia vibaya fedha zinazotokana na wafadhili ila inasemwa hivyo kutokana na kuwepo kwa wachache ambao wanakuwa na asasi za mifukoni,” alieleza Tawfiq.

Kutokana na hali hiyo, Tawfiq ameziasa asasi ambazo zimekuwa zikitembea na asasi katika mabegi waache mara moja kwani kufanya hivyo kunasababisha asasi zionekane zote hazifanye vizuri.

Mbali na hilo amezitaka asasi mbalimbali kuhakikisha wanafanya kazi karibu na waandishi wa habari ili kuweza kufanya ushirikimwema kwa lengo la kujua zaidi kile kinachofanywa na asasi mbalimbali.

Nao waandishi wa habari katika mkutano huo walisema kuwa kuna changamoto kati ya asasi na waandishi kutokana na kutokuwa na nyenzo za kutoshereza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!