Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Tozo 15 Mifugo na Uvuvi zafutwa
Habari Mchanganyiko

Tozo 15 Mifugo na Uvuvi zafutwa

Spread the love

SERIKALI imefuta tozo 15 katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ikiwa ni hatua ya kuboresha sekta hiyo na kuondoa vikwazo walivyokuwa wakikumbana navyo wavuvi na wafugaji. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Tozo hizo zilifutwa jana tarehe 13 Juni 2019, bungeni jijini Dodoma wakati Dk. Philip Mpango akiwasilisha mapendekezo ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/20.  

Tozo zilizofutwa ni tozo ya Sh. 5,000 ya vibali vya vyombo vya kusafirisha maziwa chini ya lita 51. Tozo ya Sh. 50,000 ya usajili wa vituo vya kukusanyia maziwa lita 201 kwa siku.

Tozo ya Sh. 5,000 ya usajili wa wazalishaji wa maziwa chini ya lita 51 kwa siku. Tozo ya Sh. 500,000 ya usajili wa wasambazaji wa pembejeo za maziwa. Tozo ya Sh. 15,000 ya usajili wa wafugaji wadogo wa mifugo ya nyama.

Tozo ya Sh. 50,000 ya usajili wa wafugaji wa kati wa mifugo ya nyama. Tozo ya Sh. 75,000 ya usajili wa wafugaji wakubwa wa mifugo ya nyama. Tozo ya Sh. 20,000 ya usajili wa wasimamizi wa minada ya awali;

Tozo ya Sh. 30,000 ya usajili wa wasimamizi wa minada ya upili na mipakani. Tozo ya Sh. 50,000 ya usajili wa minada ya upili na mipakani. Tozo ya Sh. 30,000 ya usajili wa wafanyabiashara wa minada ya awali.

Tozo ya  Sh. 60,000 ya usajili wa wafanyabiashara wa minada ya upili na mipakani. Tozo ya Sh. 100,000 ya usajili wa wafanyabiashara wa nyama na bidhaa zake nje ya nchi.

Tozo ya Sh. 1,000 ya kibali cha kusafirisha kuku nchini (vifaranga 100 kwa siku moja) na tozo ya Sh. 200 ya kibali cha kusafirisha kuku mkubwa nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NBC yapata tuzo ya mwezeshaji bora wa mikopo serikali Afrika

Spread the loveBenki ya NBC imepata tuzo ya Mwezeshaji Bora wa Pamoja...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!