October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kipa wa Yanga asaini miaka miwili Simba

Spread the love

ALIYEKUWA kipa wa Yanga, Benno Kakolanya amesaini rasmi mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba kuanzia msimu ujao. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kakolanya ambaye sehemu ya msimu uliopita aliitumikia Yanga  kabla ya kuafikiana na klabu yake hiyo ya zamani kuvunja mkataba sasa atakuwa mali ya Simba.

Mgogoro wa Kakolanya na Yanga ulitokana na madai ya malipo ya fedha kabla kipa huyo kujiondoa katika kikosi hicho ambapo kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera aliamua kumtimua na kugoma kumrejesha.

Kakolanya sasa amesaini mkataba huo na Simba akiwa mchezaji huru huku Simba wakinufaika na vita ya kipa huyo na Zahera.

Usajili huo una maana kwamba sasa Kakolanya anakwenda kupigania namba na kipa namba moja wa Simba na timu ya taifa, Aishi Manula na kipa namba mbili Deogratias Munishi ‘Dida.’

Wawili hao ndiyo waliokuwa makipa wa Stars wakati Kakolanya akiwa na Yanga ambapo sasa kama Simba kupitia benchi lake la ufundi litaendelea kuwa na maamuzi ya kumtumia kipa mmoja namba moja katika mechi nyingi huenda wawili hao mmoja akapoteza nafasi ya kuwa timu ya taifa.

error: Content is protected !!