Saturday , 4 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM amfuata Rais Ramaphosa Afrika Kusini
Habari za SiasaTangulizi

JPM amfuata Rais Ramaphosa Afrika Kusini

Spread the love

RAIS John Magufuli anatarajiwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa zinazotarajiwa kufanyika kesho tarehe 25 Mei 2019. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa  tarehe 24 Mei 2019 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, Rais Magufuli leo ameongozana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuhudhuria hafla hiyo.

Pia, katika safari hiyo Rais Magufuli ameambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula.

Aidha, taarifa ya Msigwa inaeleza kwamba baada ya Rais Magufuli kuhudhuria sherehe hiyo, anatarajia kufanya ziara rasmi ya kitaifa nchini Namibia ikiwemo kuzindua mtaa uliopewa jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

“Prof. Kabudi amesema baada ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule Ramaphosa, Rais Magufuli atafanya ziara rasmi ya kitaifa nchini Namibia ambako pia atazindua mtaa ulipoewa jina la Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere kwa kutambua mchango mkubwa alioutoa katika ukombozi wa taifa hilo,” inaeleza sehemu ya taarifa ya Msigwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!