Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wachimba kokoto waomba soko la uhakika
Habari Mchanganyiko

Wachimba kokoto waomba soko la uhakika

Kokoto za Doromate
Spread the love

KIKUNDI cha wanawake 36 kijulikanacho kama Loleni kilichopo Kijiji cha Mwarazi Kata ya Kibuko, Morogoro kinachojihusisha na uchimbaji wa kokoto aina ya “Doromate” kinaiomba Serikali kuona umuhimu wa kuwatafutia masoko ya bidhaa hizo kufuatia kuongeza nguvu za kuchimba mali hiyo na kukosa pa kuuzia. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Mwenyekiti wa kikundi hicho, Nuru Guruba alisema hayo jana kuwa kufuatia kupewa elimu maalum ya ujasirimali kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP- Mtandao) wameweza kujikita katika uchimbaji madini na kuongeza juhudi ya uchimbaji ambapo wameweza kupata lori mbili hadi tatu kwa wiki moja na hivyo kukabiliwa na changamoto ya masoko ili waweze kujikwamua zaidi kiuchumi.

Alisema, pia wanakabiliwa na changamoto ya kukosa vitendea kazi kwa ajili ya kupasua miamba, ukosefu wa banda maalum kwa ajili ya kujihifadhi wakati wa kugonga kokoto na choo kwa ajili ya kutunza mazingira na kujikinga na magonjwa.

Aidha alisema, tayari kikundi hicho kimeshapata eneo maalum la kuchimba madini aina ya Rubi jambo ambalo litawawezesha kujiinua zaidi kiuchumi na hivyo kusaidiana na Serikali katika kufikia uchumi wa viwanda kwa kuongeza kiwango cha uzalishaji.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake wachimbaji madini, (WIMA) Taifa, Scholastica Mchome wakati akizungumza na wanahabari katika Kijiji cha Mwirazi kata ya Kibuko wilayani humo alisema kunufaika kiuchumi kwa kugonga kokota kwa wanawake hao kumetokana na juhudi za WIMA kwa kushirikiana na TGNP-Mtandao.

Mchome ambaye amejikita katika kusimamia wachimbaji wadogo wadogo wanawake alisema kuwa kikundi cha Loleni kiliwahi kupewa mafunzo ya ujasiliamali mwaka jana na kujifunza mbinu mbalimbali za ujasirimali kutoka TGNP na jinsi ya kuongeza thamani kwa kile wanachokizalisha imesababisha kuleta hamasa kwa wanakikundi na kuanzisha mradi wa kugonga kokoto aina ya ‘’DOROMATE’’.

Alisema, kokoto hizo zinazotokana na majabali zimeweza kuwaongezea kipato kufuatia kuwa na utaratibu wa kuuza ndoo ndogo ya lita 10 kwa sh 3000 kwa wanunuzi wadogo wadogo sambamba na kuweka mchakato wa kuanza kuchimba madini kwa sasa.

Alisema kuwa kokoto hizo aina ya “Doromate “endapo zitaongezewa thamani zinafaa kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kutengeneza tarazo, matofali, dawa ya magnesium, dawa ya meno pamoja na mbolea kwa ajili ya kunyunyuzia zao la mpunga shambani.

Alisema kuwa lengo la WIMA ni kuwasaidia wachimbaji wadogowadogo wanawake hapa nchini ili kuwapa elimu ya kujitambua na kuwaunganisha na wadau mbalimbali kwa lengo la kuwapa elimu kuhusu suala zima la uchimbaji wa madini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza namna Nathwani alivyomjeruhi jirani yake

Spread the loveMSIMAMIZI wa Msikiti wa Wahindi Lohana aitwae, Ankit Dawda (32)...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

error: Content is protected !!