Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto Kabwe atinga Kisutu
Habari za SiasaTangulizi

Zitto Kabwe atinga Kisutu

Zitto Kabwe akitinga mahakamani Kisutu
Spread the love

MBUNGE wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Zuberi Kabwe, amefikishwa kwenye Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, muda huu wa mchana wa leo Ijumaa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Zitto ambaye alikamatwa akiwa nyumbani kwake, maeneo ya Masaki, anashikiliwa na jeshi la polisi tangu juzi Jumatano, kwa madai ya “uchochezi.”

Anatuhumiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu mauaji ya baadhi ya askari polisi na wananchi katika kijiji cha Mpeta, wilayani Uvinza mkoa wa Kigoma.

Zitto, mmoja wa wanasiasa wenye ushawishi mkubwa nchini, mara baada ya kukamatwa alipelekwa kwenye Kituo cha polisi cha Oysterbay, kabla ya kuhamishiwa polisi kati na baadaye kulazwa kwenye kituo cha polisi Mburahati.

Kupatikana kwa taarifa kuwa Zitto amefikishwa mahakamani, kumekuja saa chache baada ya shirika la kutetea haki za binadamu ulimwenguni – Amnesty International – kuingilia kati kwa kulitaka jeshi la polisi kumpa dhamana mtuhumiwa au kumfikisha mahakamani.

Katika taarifa yake, Amnesty limesema, ni wajibu wa vyombo vya dola nchini kumfungulia mashtaka mahakamani Zitto au kumuachia huru mara moja.

Kabla ya kukamatwa na Polisi, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno, alimtaka Zitto kuwasilisha alichokiita, “vielelezo vya madai yake,” kuwa watu zaidi ya 100 wameuwa katika eneo la Uvinza.

Zitto ambaye ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT- Wazalendo, aliwaambia waandishi wa habari wiki iliyopita kuwa wananchi zaidi ya 100 wamepoteza maisha katika vurugu zilizoibuka kufuatia mgogoro wa ardhi wilayani Uvinza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!