Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko CRDB, Mmiliki wa Batco ‘wakaliwa’ kooni
Habari Mchanganyiko

CRDB, Mmiliki wa Batco ‘wakaliwa’ kooni

Nyundo ya Hakimu
Spread the love

MAHAKAMA Kuu kanda ya Mwanza, imetupilia mbali mapingamizi mawili yaliyowekwa na wakili wa upande wa mlalamikiwa namba mbili, mfanyabiashara wa mabasi ya Batco, Baya Kusaga Malagi kwenye kesi ya mauziano ya hoteli ya Tai Five ya jijini Mwanza. Anaripoti Moses mseti, Mwanza … (endelea).

Kesi hiyo ya madai ya ardhi namba 46 ya mwaka  2017 ilifunguliwa na aliyekuwa mmiliki wa hoteli hiyo iliopo Kata ya Nyamanoro jijini Mwanza, Christopher Tarimo Mwaka 2017 Katika mahakama kuu kanda ya Mwanza.

Jaji wa Mahakama kuu kanda ya Mwanza, Jaji Issa Maige akitoa hukumu katika ya msingi kupitia mapingamizi mawili, alisema mapingamizi ya kisheria yaliyowekwa na wakili upande wa mlalamikiwa namba mbili mfanyabiashara Kusaga Malagi kuwa hayana mashiko.

Mapingamizi hayo mawili ni kufanana kwa shauri lililokuwepo mahakamani hapo mwaka 2011 na pingamizi lingine lililowekwa kuwa ni usumbufu kwa mahakama kusikiliza kesi kwa mara nyingine tena.

Upande wa mjibu maombi namba moja benki ya CRDB uliwakilishwa na wakili, Galati Silwane huku upande wa mlalamikiwa namba mbili ukiwakilishwa na wakili Emmanuel Anthony.

Kwa upande wa mlalamikaji, Christopher Tarimo uliwakilishwa na mawakili wasomi Julius Mushumbusi na Mwita Emmanuel kutoka kampuni ya wanasheria ya Kailu Law chembers.

Hata hivyo, baada ya hoja hizo kusikilizwa kwa pande zote mbili kuhusu hoja hizo, Jaji Maige alidai mahakama imeona kwamba kulikuwa na utata mkubwa katika mauziano ya hoteli ya Tai Five yaliofanyika kati ya mlalamikiwa namba moja na mbili.

Jaji alisema kuwa katika mauziano hayo pia yaligubikwa na sintofahamu nyingi kwamba mauziano hayo yalifanyika bila kukazia hukumu ya kesi namba 4 ya 2011.

Pia alisema mauziano ya wajibu maombi yanaonekana kama yalifanyika baina ya waleta maombi (Tai Five LTD na Christopher Tarimo)na mjibu maombi namba moja ( The Mogeji Instruments).

“Kwa vile mgogoro uliokuwepo katika suala hili ni kitendo cha CRDB kutoa na kuruhusu hati za Tai Five LTD na Christopher Wilson Tarimo kukopewa na Baya Kusaga Malagi bila ridhaa yake au kujulishwa hivyo mahakama imeona pingamizi zilizowekwa na upande wa mlalamikiwa hazina hazina mashiko,” alisema Jaji Maige.

Mtandao huu ulipomtafuta nje ya mahakama, Wakili wa upande mlalamikaji, Mwita Emmanuel aligoma kutoa ushirikiano bali alidai suala hilo wanaiachia mahakama yenye mamlaka ya kutenda haki.

“Mahakama tuna imani nayo na itatenda haki kwa pande zote mbili hukumu hii imeanza kuonesha mwaga, ni wazi dalili za ushindi kwa Tai Five na Tarimo zimeanza kuonekana alisema Emmanuel.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

Habari Mchanganyiko

GGML yaja na teknolojia za kisasa maonesho ya OSHA Arusha

Spread the loveKATIKA kuelimisha wananchi na washiriki wa maonesho ya usalama na...

error: Content is protected !!