Tuesday , 3 October 2023
Home Habari Mchanganyiko Asasi za Kiraia hatarini kutakatisha fedha
Habari Mchanganyiko

Asasi za Kiraia hatarini kutakatisha fedha

Spread the love

IMEELEZWA kuwa Asasi za kiraia nchini zipo katika hatari ya kutumika kama sehemu ya kupitishia fedha chafu na watu wasiokuwa na nia njema. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Hayo yalielezwa jana na Kaimu msajili wa mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali nchini Baraka Leonard, wakati alipokua akijibu baadhi ya maswali ya washiriki wa maonyesho ya wiki ya Azaki yanayofanyika jijini Dodoma.

Alisema sekta hiyo ipo katika hatari kubwa ya kutumika kama sehemu ya utakatishaji wa fedha haramu ambazo zimekuwa zikipatika katika njia zisizo sahihi.

Alisema kuwa fedha nyingi chafu zimekuwa zikingizwa nchini katika mfumo halali wa mzunguko wa uchumi pasipo kujulikana namna ambavyo zimepatikana.

“Ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa kila fedha inayoingia nchini katika Asasi zetu imekuja kutoka wapi na imeingizwa kwa misingi ipi,” alisema Leonard.

Aidha alisema kuwa kitendo cha fedha chafu kuingizwa nchini kupitia Asasi za kiraia kina madhara makubwa katika mfumo wa uchumi wa taifa.

“Tutawaletea wataalamu wa mambo haya ili waweze kuwafundisha namna ya kujikinga na kutumika kupitishiwa fedha chafu na namna ambavyo fedha hizo zilivyo na madhara katika uchumi wetu,” alisema.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto, Dk. John Jingu alisema ili kuondokana na hali hiyo Asasi za kiraia zinatakiwa kufanya kazi kwa uwazi na uwajibikaji.

Alisema kama Asasi zitafanya kazi zake kwa uwazi serikali haitakuwa na mashaka katika utendaji wao wa kila siku tofauti na ilivyo sasa katika baadhi ya maeneo.

“Tuishi kwa kufuata misingi ya sheria na utawalawa wa sheria kwa kufanya kazi kwa uwazi na uwajibikaji,” alisema Dk. Jingu.

Alisema hivi sasa kuna baadhi ya watu wanaweza kuiba fedha sehemu na kuzipeleka katika NGOs ili kuweza kuzitakatisha hivyo ni lazima Azaki kufanya kazi kwa uwazi.

“Unaweza kukuta mtu kapiga fedha sehemu au serikalini lakini kuzipeleka BOT anaogopa kuhojiwa hivyo anaona njia sahihi ya kufanya ni kufungua NGO haraka ili kuweza kuzipeleka fedha hizo na kuzitakatisha,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wawili wanaswa wakitengeneza noti bandia

Spread the loveJESHI la Polisi mkoani Songwe limewakamata watu wawili kwa tuhuza...

AfyaHabari Mchanganyiko

Chanjo mpya ya malaria Sh 5,000-10,000

Spread the loveShirika la afya la Duniani (WHO) limeridhia chanjo ya pili...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wagonjwa kiharusi waongezeka, Hospitali Mkapa yaja matibabu mapya

Spread the loveHOSPITALI ya Benjamini Mkapa kwa kushirikiana na madaktari Bingwa kutoka...

Habari Mchanganyiko

Wananchi waamua kujenga zahanati kukwepa adha kufuata huduma mbali

Spread the loveWANANCHI wa Kijiji cha Kwikerege, kilichopo katika Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!