Saturday , 10 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Elimu yapunguza ukeketaji Simanjiro
Habari Mchanganyiko

Elimu yapunguza ukeketaji Simanjiro

Spread the love

KUTOKANA na juhudi zinazofanywa na wanaharakati kwa kupinga unyanyasaji na utatili kwa watoto wa kike na akina mama na kutoa elimu juu ya madhara ya ukeketaji,  juhudi hizo zimepelekea Ukeketaji kupungua katika Wilaya ya Simanjiro. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Hayo yalielezwa  Jijini hapa na Mwanaharakati wa kupinga ukeketaji kutoka Mtandao wa kupinga madhara ya ukeketaji nchini (Nafgem) Nagalali Therritho.

Therritho alitoa maelezo hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika banda la Nafgem, katika maonesho ya wiki ya AZAKI 2018 inayofanyika kitaifa Jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa Mwanaharakati huyo,alisema awali katika eneo la Simanjiro ukeketaji ulikuwa upo juu lakini mara baada ya kufika Nafgem na kutoa elimu ukeketaji umepungua.

“Sina takwimu lakini kwa sasa ukeketaji umepungua sababu ni elimu tuliyoenda kutoa katika eneo la Simanjiro,” alisema.

Alisema yeye ni mzaliwa wa Simanjiro na alikwepa kukeketwa wakati akiwa mwanafunzi na alisaidiwa na Nafgem.

“Mimi nimesomeshwa na Shirika hili,nilitaka kukeketwa lakini wakanisaidia,sasa hivi natoa elimu na nilienda kutoa elimu, Simanjiro, japokuwa wazazi walinikataa lakini sasa hivi wamenikubali mara baada ya kuona nina kazi,” alisema.

Alisema awali mbinu iliyokuwa ikitumika kukeketa ilikuwa ni kuwakeketa watoto wakiwa wachanga.

“Mara baada ya kuona tunawabana sana wakiwa wanasoma,walikuja na mbinu nyingine ya kuwakeketa watoto wachanga,tulipambana na hili limeisha kwa sasa,” alisema.

Alisema changamoto kubwa wanayokutana nayo ni ukosefu wa maji katika eneo la Simanjiro hivyo watoto wengi kupata ugonjwa wa Lawalawa ambao husababisha uke kuwasha.

“Huu ugonjwa mtoto anawashwa kwenye uke,anakuwa anajikuna hivyo mzazi anaambiwa dawa pekee ni kukeketwa jambo ambalo sio kweli,tumetoa elimu kuhusiana na hili na wametuelewa,” alisema.

Alisema mara baada ya kuwaokoa watoto ambao walitaka kukeketwa wamewapeleka shule pamoja na katika Vyuo vya Ufundi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi zaidi ya 100 wapigwa msasa wa udereva kukabiliana na ajali

Spread the love  KATIKA kuhakikisha wimbi la ajali za barabarani zinapungua kama...

Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yakana kuhamisha kwa nguvu jamii ya Kimasai Loliondo

Spread the loveWAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro,...

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

error: Content is protected !!