Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Michezo Dreamliner yakwama kuipeleka Stars Cape Verde
Michezo

Dreamliner yakwama kuipeleka Stars Cape Verde

ATCL Dreamliner
Spread the love

SERIKALI kupitia Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Harison Mwakyembe ameeleza sababu za ndege ya serikali aina ya Dreamliner kushindwa kuisafirisha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars nchini Cape Verde, ni baada ya kukosa uwanja wa kutua ndege hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Hapo awali serikali ilitoa ndege hiyo kwa ajili ya kusafirisha kikosi hicho kinachokwenda kupambana na Cape Verde ili kuwania tiketi ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa Afrika linalotarajia kufanyika mwakani nchini Cameroon.

Baada ya kukosekana ndege hiyo Waziri Mwakyembe alisema kuwa wameongea na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) na wamefanikiwa kuagiza ndege nyingine yenye usajili wa Tanzania ambayo itabeba wachezaji pamoja na viongozi wanaotarajia kuondoka leo majira ya saa 5 usiku.

“Kiwanja cha Praia ambao ni mji mkuu wa Cape Verde ni kidogo na njia yake ya ndege ni ndogo ina urefu wa kilomita 2.1 wakati ndege yetu Dreamliner inahitaji kilomita 3 ili iweze kutua,” alisema Mwakyembe.

Mwakyembe aliongezea kuwa wachezaji wamepewa vipaji kwa ajili ya kulipambania taifa na kuleta tabasamu kwa watanzania wengine, taifa lipo nyuma ya timu na tuna hakikisha tunafuzu kwenda Cameroon ndio maana Serikali imehakikisha tunapata ndege binafsi.

Timu hiyo imeagwa mapema leo na kwenda kucheza mchezo wake wa tatu katika kundi L, siku ya Ijumaa 12, Octoba 2018 dhidi ya Cape Verde na siku nne baadae watacheza mchezo wa marudiano kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa tu kutoka Meridianbet

Spread the love  IKIWA leo hii ni Jumamosi nyingine na tulivu kabisa,...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

error: Content is protected !!