Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mauaji, ubaguzi wa mawakala dosari uchaguzi wa marudio
Habari za SiasaTangulizi

Mauaji, ubaguzi wa mawakala dosari uchaguzi wa marudio

Salum Mwalimu, Mgombea Ubunge KInondoni (Chadema) akihoji uchaguzi kuendelea baada ya sanduku la kura kuibwa na kurudishwa kituoni
Spread the love

KITUO cha sheria na Haki za Binaadamu (LHRC) kimeeleza mauaji, kubaguliwa kwa mawakala wa upinzani kumetia dosari uchaguzi wa marudi wa jimbo la Kinondoni na Siha pamoja na Kata 10. Ananaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizingumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi wa kituo hicho, Anna Henga amesema kuwa mauji yalijitokeza kipindi cha kampeni za uchaguzi wa jimbo la Kinondoni yameupa sura mbaya uchaguzi huo.

Uchaguzi katika majimbo ya Kinondoni na Siha umefanyika baada ya wabunge wake Maulidi Mtulia aliyekuwa mwanachama wa CUF na Dk. Godwin Mollel wa Chadema, kujiuzulu na kuhamia CCM na wote kugombea tena kwenye uchaguzi uliitwa na Tume ya uchaguzi nafasi hiyo hiyo kupitia (CCM) .

Henga amesema kuwa kwenye uchaguzi huo kuliibuka matumizi ya nguvu yaliyopelekea watu kuujeruhiwa na kuuwawa.

“Katika Jimbo la Kinondoni Februali 16, mwaka huu, mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini aliuwawa kwa kupigwa risasi kutoka na Polisi kufyatua risasi kwenye maandamano ya wafuasi wa Chadema walikuwa wakidai viapo vya mawakala wao.

Amesema kuwa jeshi hilo liliwashikiria liliendelea kuwashikiria wafuasi 40 wa Chadema wakiwepo wanawake wenye watoto wadogo na majeruhi wawili wa risasi. “Siha Polisi walimpiga mtu mmoja aliyefahimika kwa jina la Husna Saidi na kupelekea kumvunja Mguu”

Pia amekitaja kifo cha Katibu wa Chadema kata ya Hananasif, Daniel John ambapo amedai kuwa kampeni hizo ziliiacha machungu kutokana na vifo hivo.

Henga amesema kuwa kituo hiko kilishuhudia unyanyasaji wa mawakala wa vyama vya siasa. “Siku ya uchaguzi waangalizi wa (LHRC) walishuhudia baadhi ya mawakala wakinyanyaswa na kuzuiliwa kuingia kwenye vituo vya kupiga kura kwa madia kuingia na viapo vilivyokosa saini ya Mkurugenzi wa uchaguzi na wengine kuwa na nakala.”

“Katika Jimbo la Siha hali hiyo ilishuhudiwa kwenye kituo cha Nasai shule ya msingi ambapo mawakala wa CUF na Sauti ya Umma (Sau) na Chadema walizuiliwa kuingia kwenye kituo bila sababu za msingi,” amesema Anna Henga.

Katika Jimbo la Kinondoni Kituo hiko kilishuhudia mawakala wa Chadema kutopewa viapo vyao kwa wakati iliyopelekea kusumbuliwa siku ya uchaguzi.

Amesema kuwa wasimamizi wa uchaguzi waliwazuia waangalizi wa uchaguzi huo kutoingia ndani ya vituo hivyo ambapo ni kinyume na sheria ya uchaguzi kifungu namba 63 (1)f cha sheria ya uchaguzi sura namba 343.

Amesema licha ya baadhi ya vituo kutokuwa na mazingira rafiki kwa wapiga kura kutokana kuwepo kwa vituo ambavyo vilikosa usiri wa mpiga kura wakati alipokuwa akipiga kura.

Henga amesema dosari nyingine ni kuibwa kwa sanduku la kupiga kura na kurejeshwa kwenye kito cha Magomeni Idrisa bila kuchukuliwa hatua yoyote.

Amesema kuwa LHRC ilishuhudia matumizi ya watoto kwenye kampeni ambapo ni kinyume cha sheria namba 12 cha sheria ya mtoto 2009 .

Kituo cha sheria ya Haki za binadamu kilishuhudia video ya mtoto aliyepandishwa kwenye jukwaa la kampeni za mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Maulidi Mtuliya kwenye kata ya Makumbusho.

Hanga amesema kwenye kampeni za uchaguzi huo baadhi ya viongozi wa umma walitumia gari za umma kwenye misafara ya kampeni ilhali ni kinyume cha sheria ya uchagazi na vyama vya siasa.

Amesema kituo hiko kimeshuhudia Viongozi wa Umma katika Jimbo la Siha wakitumua gari za umma katika Kampeni za Mgombea katika jimbo hilo kwa tiketi ya CCM Dk Mollel ambapo alionekana Waziri wa Adhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akiwa kwenye kampeni hizo akitumia gari za umma.

Hanga amesema kituo hiko kimebaini muitukio mdogo wa wapiga kura tofauti na ule idadi ya watu waliojiandikisha na wale waliokuwa wakijitokeza kwenye kampeni.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!