Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ndugai uso kwa uso na Lissu, kupelekwa Ulaya J’mosi
Habari za SiasaTangulizi

Ndugai uso kwa uso na Lissu, kupelekwa Ulaya J’mosi

Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki akiwa katika hospitali ya Nairobi kwa matibabu. Picha ndogo Spika wa Bunge Job Ndugai
Spread the love

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, anatarajiwa kufika mjini Nairobi leo au kesho Alhamisi kumtembelea mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu. Anaripoti Mwandishi Wetu kutoka Nairobi….(endelea).

Taarifa kutoka Bunge la Tanzania na familia ya Lissu jijini Dar es Salaam na mkoani Singida zinathibitisha kuwa Ndugai atakwenda Nairobi kumjulia hali Lissu na kupata taarifa ya matibabu yake.

“Ni kweli kuwa Spika Ndugai atakwenda Nairobi kati ya leo (Jumatano) na kesho Alhamisi kumuona mheshimiwa Lissu. Mipango ya safari hiyo inaratibiwa na familia ya Lissu na baadhi ya marafiki zake wa karibu,” ameeleza mmoja wa wanafamilia wa mbunge huyo.

Amesema, “Ndugai anakwenda Nairobi kuonana na Lissu, kwa lengo la kuzunguza naye juu ya matibabu yake. Anakwenda kwa lengo la kujua maendeleo ya afya ya mbunge huyo na jinsi alivyoathirika na majeraha ya risasi.”

Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja kipindi ambacho, Lissu amekuwa akinukuliliwa kulalamikia Ndugai kuwa “amemtekeleza” Nairobi.

Spika huyo wa Bunge, hajakwenda Nairobi kumuona mbunge wake, tangu mwanasiasa huyo kupelekwa mjini humo Septemba mwaka huu.

Lissu alishambuliwa kwa risasi za moto na wanaoitwa na serikali, “watu wasiofahamika,” nyumbani kwake, majira ya saa saba na nusu mchana akiwa ndani ya gari eneo la Area D, mjini Dodoma.

Kabla ya kupelekwa Nairobi, Lissu alitibiwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma.

Taarifa kutoka familia ya mwanasiasa huyo na Lissu mwenyewe zinasema, mbunge huyo wa Singida Mashariki, anatarajiwa kuondoka mjini Nairobi, Jumamosi wiki hii.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Lissu anapelekwa moja ya nchi za Ulaya, jina na hospitali anayokwenda tunaihifadhi kwa sasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

error: Content is protected !!