Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Watu wasiojulikana’ wanyemelea roho ya Lema
Habari za Siasa

‘Watu wasiojulikana’ wanyemelea roho ya Lema

Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini
Spread the love

MBUNGE wa Arusha mjini, Godbless Lema (Chadema), amefunguka na kueleza anavyowindwa na watu wasiojulikana kama ilivyotokea kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu (Chadema), anaandika Faki Sosi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Lema amesema anaishi kwa mashaka kutokana na kuwindwa na watu wasiojulikana.

Hivi karibuni viongozi wa Chama hicho wameeleza kuwa wanatishiwa uhai wao ingawa Jeshi la Polisi halijachukua hatua zozote kuhusu madai hayo.

Ametupia lawama Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kwamba wameshindwa kuchukua hatua na hivyo wanatakiwa kuachia ngazi.

Lema ameeleza kuwa imefikia hatua anaogopwa na familia yake kutokana na kuonekana kuwa muda wowote atapigwa bomu au risasi.

Amesema kuwa kama serikali ya Rais John Magifuli haijui nani anayefanya matukio haya basi naye hayupo salama.

“Kama serikali ya Rais Magufuli haijui nani anayefanya matukio haya yeye mwenyewe hayupo salama kama yeye mwenyewe hayupo salama kwanini anarelax ? (kupumzika) kama hajui nani anafanya matukio haya anamwachaje Sirro kazini, anamwachaje Kipilimba kazini, watu wanapigwa risasi, maiti zinaokotwa, “ ameeleza

Mkuu wa Operesheni na mafunzo ndani ya Chadema Benson Kigaila, amesema kuwa tukio la Tundu Lissu alijitokeza kijana ambaye alitangaza kuomba ruhusa ya kutaka kumuua mbunge huyo lakini hakukamatwa.

Kigaila amesema uchunguzi wa jeshi la Polisi ungeanza kwa kijana huyo ambaye amekuwa akijinadi lakini polisi wapo kimya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!