Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko January Makamba ‘amchokonoa’ Dk. Mengi
Habari Mchanganyiko

January Makamba ‘amchokonoa’ Dk. Mengi

Januari Makamba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais, Mazingira na Muungano. Picha ndogo, Reginald Mengi
Spread the love

JANUARY Makamba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, amedai kuwa vyombo vya habari vya kampuni ya IPP Limited chini ya Dk. Reginald Mengi, vimekuwa ‘vikimtenga’ tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu nchini, mwaka 2015, anaandika Charles William.

Dk. Mengi ni Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya IPP Limited, inayomiliki vyombo mbalimbali vya habari, ikiwemo vituo vya runinga vya ITV, EATV, Capital, vituo vya redio; Capital radio, Radio One stereo, East Africa radio na magazeti ya Nipashe, The Guardian na vinginevyo.

Katika andiko lake, kupitia ukurasa wa Twitter Makamba amemwambia Dk. Mengi kuwa, “Kipindi cha kampeni, vyombo vyako vya habari vilikuwa upande mwingine, na mpaka sasa, nimefungiwa katika vyombo hivyo kutokana na kazi niliyofanya wakati wa kampeni.”

Ujumbe wa Makamba kwa Dk. Mengi, umekuja masaa machache baada ya mfanyabiashara huyo, kuweka mtandaoni moja ya hotuba za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na kuandika, “Hayati Nyerere alitabiri ujio wa Rais (John) Magufuli. Naamini Rais Magufuli hawezi kugeuka jiwe.”

https://twitter.com/JMakamba/status/904457857323687937

Mpaka sasa, Dk. Mengi hajajibu maneno hayo ya Makamba. Ingawa baadhi ya wachangiaji katika mtandao huo, wameshangazwa na madai ya Makamba kuwa, vyombo vya habari vya IPP vilikuwa vikiegemea upande mmoja katika kampeni za mwaka 2015.

“IPP hawakuwa na upande katika na kuripoti mambo kama yalivyo bila kupendelea. Kitu ambacho wananchi tunapenda,” amejibu Spaita S. Ndelwa, mmoja kati ya wachangiaji.

Huku mtoa maoni mwingine mwenye jina la Ednxie akisema, “TBC1, TBC2, Star TV na ZBC walikuwa upande wenu (CCM), ila IPP kupitia ITV walikuwa hawana upande.”

Itakumbukwa kuwa January Makamba, ambaye pia kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, mkoani Tanga ndiye alikuwa msemaji wa timu ya kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

Habari Mchanganyiko

GGML yaja na teknolojia za kisasa maonesho ya OSHA Arusha

Spread the loveKATIKA kuelimisha wananchi na washiriki wa maonesho ya usalama na...

error: Content is protected !!