Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko BoT yakumbushwa kudhibiti fedha haramu
Habari Mchanganyiko

BoT yakumbushwa kudhibiti fedha haramu

Benki Kuu ya Tanzania
Spread the love

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imetakiwa kufuata muongozo wa fedha unaokubalika ili kudhibiti fedha haramu zisiingie katika mzunguko halali, anaandika Mwandishi Wetu.

Aidha, kupitia muongozo huo BoT itafahamu fedha zinazoingizwa nchini na kufahamu zinaingia kwa njia gani.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar, Dk. Khalid Salum Mohammed wakati akifungua kikao cha siku tano cha taasisi ya kudhibiti utakasishaji wa fedha haramu kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika uliofanyika visiwani Zanzibar.

“Upo muuongozo wa fedha ambao umekubalika katika kupambana na utakatisishaji wa fedha haramu kwa hivyo BoT inatakiwa kufuatilia hatua kwa hatua utekelezaji wake,” amesema.

Aidha, Dk. Mohammed alishauri kwamba ni vyema mabenki kujuwa wateja wao na kuzifahamu kazi zao kabla ya kuingiza fedha katika benki ili kuweza kuzitambuwa kama fedha haramu au halali.

Amesema awali walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya kutunga sheria za kimataifa za kupambana na fedha haramu kwa nchi moja moja na kwamba hivi sasa wanatumia sheria zinazofanana.

Amesema fedha haramu zinazotokana na biashara za dawa za kulevya na usafirishaji wa binadamu hutumika kufadhili shughuli za kigaidi hivyo kuna umuhimu mkubwa kwa taasisi za kifedha kudhibiti masuala hayo.

Ameongeza kuwa fedha hizo huko zinakotoka huwa hazitumiki na kwamba husafirishwa na kuletwa Afrika au Tanzania ili kuwekezwa katika mahoteli na baadaye kurudi katika nchi zilizotoka fedha hizo na kuonekana ni fedha halali.

“Biashara hii inaweza kusababisha Benki kufa na uchumi unaweza kuathirika kwa sababu wakati mwIngine fedha hizi zinakuja kwa wingi na zinaweza kuwafukuza wawekezaji hivyo ni muhimu kuwa na nguvu za pamoja ili kuondokana na tatizo hili,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

Habari Mchanganyiko

Yara yaja na bima ya mazao kwa wakulima

Spread the love  WAKATI serikali ikiweka mikakati mbalimbali kuimarisha sekta ya kilimo...

error: Content is protected !!