Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania yatangaza kushiba chakula
Habari Mchanganyiko

Tanzania yatangaza kushiba chakula

Mahindi
Spread the love

SERIKALI  imesema kuwa Taifa kwa sasa linajitosheleza kwa chakula kwa asilimia 120 kulingana na tathmini iliyofanyika mwaka huu, anaandika Mwandishi wetu.

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Waziri  wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba  katika mashindano ya mifugo kitaifa yanayofanyika uwanja maonesho ya Nanenane Nzuguni, mjini Dodoma.

Anasema kutokana na tathmini iliyofanyika katika msimu huu wa kilimo inaonesha kuwa Tanzania inajitosheleza kwa chakula kwa asilimia 120.

“Kwa sasa chakula kilichopo kinatutosha sasa wale watanzania wenye tabia ya kuuza chote na kwenda kwa Wakuu wa mikoa au wilaya kusema hawana chakula taratibu huo haupo,”anasema Tizeba

Anawataka kutouza chakula chote kwani kufanya hivyo ni kusababisha familia kuwa na uhaba wa chakula.

“Utaona mtu ana gunia nne halafu anazipeleka zote sokoni kwa kutegemea kuliamsha mbele ya safari, halitaamka,” alisisitizaTizeba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!