SERIKALI imesema kuwa Taifa kwa sasa linajitosheleza kwa chakula kwa asilimia 120 kulingana na tathmini iliyofanyika mwaka huu, anaandika Mwandishi wetu.
Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba katika mashindano ya mifugo kitaifa yanayofanyika uwanja maonesho ya Nanenane Nzuguni, mjini Dodoma.
Anasema kutokana na tathmini iliyofanyika katika msimu huu wa kilimo inaonesha kuwa Tanzania inajitosheleza kwa chakula kwa asilimia 120.
“Kwa sasa chakula kilichopo kinatutosha sasa wale watanzania wenye tabia ya kuuza chote na kwenda kwa Wakuu wa mikoa au wilaya kusema hawana chakula taratibu huo haupo,”anasema Tizeba
Anawataka kutouza chakula chote kwani kufanya hivyo ni kusababisha familia kuwa na uhaba wa chakula.
“Utaona mtu ana gunia nne halafu anazipeleka zote sokoni kwa kutegemea kuliamsha mbele ya safari, halitaamka,” alisisitizaTizeba.
Leave a comment