Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Maambukizi ya VVU yapiga kambi kwa wanandoa
Habari Mchanganyiko

Maambukizi ya VVU yapiga kambi kwa wanandoa

Spread the love

WATU waliofunga ndoa na kuunganika kuwa kama mwili mmoja na kuepukana na masuala ya kufanya ngono zembe, imebainishwa wao kwa sasa ndio wamekuwa vinara wa kupata maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), kutokana na kutozingatia sheria na kanuni za ndoa, ananadika Mwandishi Wetu.

Imeelezwa kuwa watu wamekuwa wakiingia kwenye ndoa kama fasheni, bila ya kufahamu nini maana ya kufunga pingu hizo za maisha, na kujikuta baada ya muda mfupi wamechokana na kuanza kufarakana.

Hayo yalizungumzwa juzi na mwandishi wa kitabu cha Sakramenti ya ndoa katika nyumba aminifu Paschal Maziku, wakati akikitambulisha kwa waumini wa Kanisa Katoliki mjini Shinyanga.

“Tulifanya utafiti na kugundua wanandoa ndio wamekuwa vinara wa maambukizi mapya ya VVU, ambapo kisheria wanandoa ndio wanapaswa kuwa salama sababu kabla ya kufunga pingu za maisha huwa wanapimwa afya zao, lakini kwa hali ya sasa imebadilika na wengi wao ndio
waathirika wa Ukimwi,” amesema Maziku

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

error: Content is protected !!