Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto Kabwe aipongeza serikali ya Magufuli
Habari za Siasa

Zitto Kabwe aipongeza serikali ya Magufuli

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT
Spread the love

MBUNGE wa Jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameipongeza Serikali kwa kuifanya Kigoma kuwa bandari ya mwisho kwa mizigo inayokwenda Kongo na Burundi, anaadika Mwandishi Wetu.

Kabwe alitoa pongezi hizo wakati akizungumza na Mawaziri wa Tanzania, Kongo, Burundi, Zambia na Uganda katika ukumbi wa Lake Tanganyika jana.

Alisema hivyo uchumi wa Kigoma utaongezeka kwa kiasi kikubwa kwa sababu Burundi peke yake inaagiza mizigo kupitia bandari ya Dar es salaam zaidi ya tani 350, 000.

“Mimi napenda niipongeze sana serikali yetu kwa kuweza kufanya kazi kwa pamoja na wenzetu wa nchi za jirani kama Burundi, Kongo, Zambia na Uganda kwa kuweza kukubaliana maazimio waliyokubaliana katika mkutano huu.

Jambo la msingi ambalo napenda kulisisitiza ni kuimarisha reli kwa sababu kama tunataka mzingo uweze kufika Bukavu kwa harakakupitia bandari ya Kigoma lazima reli ya kati ifanye kazi vizuri”alisema Zitto.

Alisema kama reli ikifanya kazi vizuri hapo ndipo uchumi wa Kigoma utakuwa sana kwa sababu mtu akisafirisha mizigo kutoka Dar es salaam kwa reli hadi Kigoma itakuwa ni raisi sana kuliko kuisafirisha kwa barabara.

Alisema serikali ikiimarisha reli ya kati mzunguko wa fedha katika mkoa wa kigoma utaongezeka sana na kufanya watu kujenga mahoteli, watazalisha chakula na kutumia fedha za hapa na hivyo kudumisha mkoa wa Kigoma.

“Kwa hiyo sisi ambao tumekulia hapa Kigoma ni jambo la historia pia nawapongeza Mawaziri wote ambao wameshiliki katika mkutano huu pamoja na serikali zote kufanya Kigoma kuwa lango kuu wa biashara.

Aidha Mawaziri waliyohudhulia mkutano huo ni Makame Mbarawa wa Tanzania, John Bosco wa Burundi, Aggrey Bagire wa Uganda, Niyonkuru Pelalte wa Burundi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

Serikali kuongeza wanufaika mikopo ya elimu ya juu

Spread the loveSERIKALI imesema itaongeza idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kufumua mitaala ya vyuo vikuu, ufundi stadi

Spread the loveSERIKALI inakusudia kufanya mapitio katika mitaala na programu za vyuo...

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

error: Content is protected !!