Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko ALAT kuhamia mkoani Dodoma mwezi ujao
Habari Mchanganyiko

ALAT kuhamia mkoani Dodoma mwezi ujao

Mwenyekiti wa ALAT taifa, Gulamhafeez Mukadamu (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
Spread the love

JUMUIYA ya Tawala ya Mitaa (ALAT) Tanzania inatarajia kuhamia mkoani  Dodoma ifikapo tarehe 1 mwaka huu, ikiwa ni  sehemu ya kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kuzitaka serikali kuhakia mkoani humo, anaandika Catherine Kayombo.

Mwenyekiti wa ALAT taifa, Gulam hafeez Mukadam, ametoa taarifa hiyo katika mkutano na wanahabari uliofanyika leo  idara ya habari na maelezo jijini Dar es salaam.

“Naunga mkono juhudi za rais kwa vitendo kwa kuhamishia shughuli za serikali makao makuu Dodoma, ambapo ALAT kuanzia tarehe mosi Agosti, 2017 ofisi za makao makuu zitahamia Dodoma”, alisema Mukadamu.

Katika mkutano huo, mwenyekiti  pia amekemea watumishi wa ALAT wasio waadilifu na kutoa taarifa ya hatua zitakazochukuliwa ili kuhakikisha kurejesha amani kwa wanajumuiya.

“Hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa watumishi wa sekretariat ya ALAT makao makuu ambao siyo waadilifu na wenye utendaji kazi usioridhisha”, aliongeza.

Mukadamu ametoa rai kwa mamlaka za serikali za mitaa kuendelea kuchangia chombo chao cha ALAT  kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi kwa manufaa ya wananchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!