Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Anna Mghwira akabidhiwa Ilani CCM, ACT kumjadili
Habari za SiasaTangulizi

Anna Mghwira akabidhiwa Ilani CCM, ACT kumjadili

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rodrick Mpogolo (kushoto) akimkabidhi ilani ya CCM Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira.
Spread the love

ANNA Mghwira, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo amekabidhiwa Ilani ya CCM baada ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Ikulu leo, anaandika Hamisi Mguta.

Mghwira amekabidhiwa Ilani hiyo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara) Rodrick Mpogolo ikiwa ni sehemu ya Katiba ya CCM, kuwa Mkuu wa Mkoa ni sehemu ya chama hicho na anashiriki kikao cha kamati ya siasa ya mkoa.

Kutokana na tukio hilo Uongozi wa chama cha ACT-Wazalendo kesho inatarajia kukutana kutafakari namna Anna Mghwira, Mwenyekiti wa chama hicho atakavyotekeleza majukumu ya nafasi hiyo na Ukuu wa mkoa.

Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa chama hicho amesema uamuzi huo ni baada ya Mghwira kufanya mazungumzo na viongozi wenzake wa juu wa chama kuhusu uteuzi wake.

Anna Mghwira muda mchache baada ya kuapishwa mapema Ikulu leo

“Kufuatia uteuzi huu na kwa kuzingatia unyeti na majukumu ya mkuu wa mkoa, Kamati ya Uongozi wa chama itakutana Juni 7, 2017 kutafakari pamoja na mambo mengine, namna ambavyo mama Anna Mghwira atatekeleza wajibu wake wa uenyekiti wa chama na majukumu yake mapya,” amesema.

https://www.youtube.com/watch?v=qPRUYeWzcXY

Mgwira ambaye alikuwa mmoja wa wapinzani wa Rais Magufuli katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 anachukua nafasi aliteuliwa na rais kushika wadhifa huo Juni 3, mwaka huu.

Anna Mghwira akiapa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mbele ya Rais John Magufuli

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kuwa uteuzi huo ni anguko kwa ACT-Wazalendo kwani Mkuu wa Mkoa anatambulika kama Mjumbe wa Kamati ya siasa (CCM) hivyo Mghwira atalazimika kukiacha chama hicho na kutimkia CCM.

Ikumbukwe kuwa uteuzi huo ndani ya chama hicho ni wa pili unafanyika na Rais Magufuli kuingiza wapinzani katika serikali baada ya Prof. Kitila Mkumbo aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!