Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge walia kupunjwa fedha zao
Habari za Siasa

Wabunge walia kupunjwa fedha zao

Bunge likiendelea na vikao vyake
Spread the love

BUNGE la Jamhuri ya Muungano limetenga Jumla ya Sh 121 bilioni kwa matumizi ya mwaka 2017/18 kutoka Sh 99 bilioni zilizokuwa zimetengwa mwaka 2016/17, lakini wabunge wamedai hazitoshi, anaandika Dany Tibason.

Hata hivyo mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Lucy Magereli amesema hakuna ufanisi katika utendaji kazi kwa shughuli za bunge mambo mengi yanakwama kutokana na uhaba wa fedha kusababisha wabunge kushindwa kutimiza majukumu yao.

Katika swali la nyongeza amesema kumekuwa na mipango ya makaratasi ndani ya bunge lakini utekelezaji wake umekuwa ni shida ambapo huwafanya wabunge wasafiri wakati mwingine kwa kutumia magari madogo ya abiria lakini siku za kazi zimepunguzwa na muda wa kuchangia bungeni umepunguzwa.

Katika swali la msingi Magereli amesema katika kipindi cha serikali ya awamu ya tano kumekuwa na mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa shughuli za Bunge kwa kupunguza muda.

“Bunge sasa hukaa kwa siku 10 hadi 12 tu, jambo ambalo linasababisha muda wa kuchangia na Mawaziri kujibu hoja kuendelea kupunguzwa hadi kufikia dakika tano kitu ambacho kimepunguza kabisa ufanisi wa chombo hichi muhimu chenye majukumu muhimu,” amesema Magereli.

Amesema kanuni za bunge zinaelekeza muda wa kamati kuelekea bajeti ni wiki tatu lakini safari hii wiki moja imeondoshwa. Muda wa uendeshaji shughuli za bunge umepunguzwa mno, kwa hiyo wabunge wanashindwa kutekeleza wajibu weao kama bunge kutokana na kukimbizana na muda.

Akijibu swali la msingi, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema mpango wa serikali kuliwezesha Bunge kufanya shughuli zake kwa ufanisi ni kutoa fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali kwenda kwenye Mfuko wa Bunge fungu 40 kwa kuzingatia bajeti iliyoainishwa na Bunge.

Dk. Mpango amesema taarifa ya utekelezaji ya Mfuko wa Bunge na hali ya upatikanaji wa fedha kifungu cha 45 (b) cha sheria ya Bajeti kinaelekeza hivyo na ndivyo wakatakavyofanya.

“Serikali inaahidi kutoa fedha zote zilizobaki kwenye bajeti ya fungu hili Sh 8.3 bilioni kwa ajili ya matumizi mengineyo na Sh. 6.7 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambazo zitatolewa kabla ya Juni 30, mwaka huu,” amesema

Hata hivyo majibu hayo alikataliwa na mbunge na hivyo Naibu Spika akaamuru swali hilo lirudiwe kujibiwa upya kwa kufuata utaratibu mzuri wa kikanuni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

error: Content is protected !!