Friday , 1 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yawachongea Waganga kwa wabunge
Habari Mchanganyiko

Serikali yawachongea Waganga kwa wabunge

Kituo cha Afya cha Kishapu
Spread the love

WABUNGE wameelezwa kuwa kiasi cha Sh. 20 bilioni hazikutumika ambazo ni za mfuko wa pamoja wa afya ujulikanao kama ‘Basket Fund’ kwa mwaka 2016/17, anaandika Dany Tibason.

Kufuatia hali hiyo, Wabunge wametakiwa kuhakikisha wanawabana Waganga wakuu wa Wilaya na wahasibu katika halmashauri zao ili fedha za mfuko huo zitumike kununulia dawa na vifaa tiba.

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Ester Mahawe.

Mahawe alitaka kujua iwapo serikali haioni umuhimu wa kupandisha bajeti ya Hospitali za Wilaya zilizoko mkoani Manyara ambazo zimekuwa zikipata ugumu katika kutoa huduma kwa wananchi.

“Vituo vya Afya na Zahanati zilizo karibu na Hospitali za Wilaya zina changamoto ya utoaji huduma bora kwa sababu ya upungufu wa dawa na watumishi wa kada ya afya hivyo kupeleka kuhudumiwa na hospitali za Wilaya ambazo bajeti ya dawa haikidhi mahitaji,” amesema Mahawe.

Akijibu maswali hayo kwa pamoja, Jafo amesema kuna tatizo la usimamizi wa rasilimali fedha ambapo katika mwaka 2016/17 mpaka mwezi wa saba kuna fedha za mfuko huo hazijatumika ambazo ni jumla ya Sh. 20 bilioni.

Alitaja mkoa wa Manyara pekee kuwa takriban Sh. 500 milioni hadi mwezi wa saba mwaka jana zilikuwa hazijatumika jambo linaloonyesha kuwa kuna mambo aliyoyaita ya hovyo kwa baadhi ya watumishi katika halmashauri mbalimbali nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Habari Mchanganyiko

4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Spread the loveWATU wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo...

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

error: Content is protected !!