Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Busara itumie kudai michango kwa wananchi
Habari Mchanganyiko

Busara itumie kudai michango kwa wananchi

Wafigaji
Spread the love

MKUU wa wilaya ya Bahi, Dodoma, Christina Kitundu, amewataka viongozi wasiwachangishe wananchi pesa za maendeleo kwa nguvu badala yake watumie busara, anaandika Dany Tibason.

Mkuu huyo wa wilaya amelazimika kutoa kauli hiyo kutokana na kuwepo kwa mvutano mkali na malalamiko kati ya viongozi wa chama cha wafugaji na uongozi wa kijiji cha Mpamatwa wilayani humo.

Kiongozi wa chama cha wafugaji kijiji cha Mpamantwa, Samweli Salon amesema uongozi wa kijiji kimekuwa kikiwatishia wafugaji kwa kuwapeleka polisi au mahakamani wasipochanga fedha za madawati.

Samweli amesema uongozi wa kijiji cha Mpamatwa wamekuwa wakiwatishia kuwapeleka polisi hata mahakamani kwa kulazimisha michango ya kutengeneza madawati.

Kiongozi huyo amesema uongozi wa serikali ya kijiji cha Mpamantwa wamekuwa wakiwatishia viongozi wa chama cha wafugaji kwa kuwapeleka polisi au mahakamani pale watakapokuwa wameshindwa kukamilisha michango ya madawati.

Samweli amesema viongozi hao wa serikali wamekuwa wakilazimisha wafugaji kulipa Sh.1,000 kwa kila kichwa cha ng’ombe na punda huku wakitaka kulipa Sh. 500 kwa kila kichwa cha mbuzi na kondoo.

Amesema mpaka sasa wanachama wa chama cha wafugaji kijiji cha Mpamantwa ni wanachama 14 ambao hawawezi kuchangia dawati 30 kama uongozi wa serikali ya kijiji inavyotaka.

“Serikali ya kijiji cha Mpamantwa walituita viongozi wa chama cha wafugaji wakitaka tuchangie madawati 30 lakini viongozi hao walilazimisha kutoza mchango wa Sh.1,000 kwa kila kichwa cha ng’ombe na punda na Sh. 500 kwa kila kichwa cha mbuzi na kondoo,” amesema Samweli.

Amesema chama cha wafugaji kiliweza kuchangishana Sh. 220,000 ambazo walizipeleka katika ofisi ya Serikali ya kijjiji ambapo viongozi hao walikataa fedha kutoka chama cha wafugaji na kuwalazimisha kuwa wasipokamilisha michango hiyo watapelekwa mahakamani.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa serikali ya kijini cha Mpamantwa, Bosco Emmanuel amesema kwamba ni kweli chama hicho kinatakiwa kuchangia madawati 30 lakini ni mchango wa hiari na hakuna kiongozi wa serikali ya kijiji ambaye atawapeleka mahakamani au polisi viongozi wa chama cha wafugaji.

Amesema tatizo ni kwamba wafugaji hao wanapungua siku hadi siku jambo ambalo linaonesha kuwa chama hicho hakiwezi kukamilisha madawati hayo kwa wakati ukizingatia suala la madawati limeisha pita muda wake.

Kutokana na hali hiyo Mkuu wa wilaya amesema siyo sahihi michango ya maendeleo kuchangiza kwa nguvu na badala yake wananchi washirikiswe na kupewa elimu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

error: Content is protected !!