Saturday , 10 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Mfuko wa PTF kunufaisha vijana Morogoro
Habari Mchanganyiko

Mfuko wa PTF kunufaisha vijana Morogoro

Mji wa Morogoro
Spread the love

MFUKO wa Rais wa Kujitegemea (PTF) umewataka vijana wakiwemo waliohitimu vyuo vya ufundi stadi na taasisi zingine, kuitumia vyema fursa ya mikopo inayotolewa na mfuko huo ili kukuza mitaji na kuongeza kipato na ajira miongoni mwao, anaandika Christina Haule.

Meneja wa PTF Kanda ya Morogoro, Christopher Peter amesema mfuko huo unaohusika na masuala ya kutoa mikopo kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ili kumfanya mtanzania mwenye uwezo wa kufanya kazi za uzalishaji afanye hivyo kwa faida yake na jamii kwa ujumla ili kukuza uchumi.

Amesema tayari zaidi ya kiasi cha Sh. 1.9 bilioni zimegawiwa kwa walengwa 5,370 kama mikopo katika kipindi cha mwaka wa fedha 1993/94 hadi mwaka 1996 kabla ya muundo mpya.

Aidha Peter amesema kuwa mfuko huo umefanikiwa kutoa mafunzo kwa jumla ya watu 995 katika kipindi cha mwezi Julai 2015- Februari 2017 wakiwemo wanawake 605, vijana 374 na kundi maalum 16.

Amesema baada ya mafunzo hayo mfuko huo umefanikiwa kutoa mikopo nafuu yenye thamani ya Sh. 426 milioni kwa makundi yaliyolengwa yenye watu 567 kwa kipindi cha mwezi Julai 2015- Februari 2017.

Amefafanua kuwa kati ya mikopo hiyo vijana 110 walipewa mikopo yenye thamani ya Sh. 99 milioni, wanawake 441 walipewa mikopo yenye thamani ya Sh. 320 milioni wakati kundi maalumu, lenye watu wenye ulemavu na wanaoishi na VVU 16 walipewa mikopo ya thamani ya Sh. 7.05 milioni wote wakiwa ni wakazi wa kata na vijiji mbalimbali ndani ya Manispaa ya Morogoro.

Amesema, mpaka sasa kiasi cha Sh. 261 milioni kimekusanywa ikiwa ni asilimia 98 ya marejesho yaliyopangwa kukusanywa kutoka kwa waliokopeshwa.

Hata hivyo wateja waliopewa mikopo hiyo ni wale wenye kushughulika na shughuli za uzalishaji mali na ubunifu na si ya uchuuzi ingawa mfuko huo umeshaanza kujikita kukuwapa mafunzo wachuuzi ya kujikita zaidi katika uzalishaji ili nao waweze kufaidika.

Mmoja wa wanufaika wa mikopo hiyo, Mohamed Msangi, Mkurugenzi Mtendaji wa Mwale Cleaner amesema amenufaika na mfuko huo kufuatia kupata mafunzo kadhaa yaliyomuwezesha kuimarika hadi kufungua ofisi rasmi mwaka 2016 iliyopo katika kata ya Kilakala Manispaa ya Morogoro.

Msangi amesema, kwa sasa wanaaminika na kupewa ushirikiano na wakazi wa kata hiyo ambapo tayari ameshinda zabuni katika kata za Kilakala na Kichangani na kufanikiwa kuongeza wanachama kutoka saba mpaka 14 huku wakiwaajiri wengine saba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi zaidi ya 100 wapigwa msasa wa udereva kukabiliana na ajali

Spread the love  KATIKA kuhakikisha wimbi la ajali za barabarani zinapungua kama...

Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yakana kuhamisha kwa nguvu jamii ya Kimasai Loliondo

Spread the loveWAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro,...

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

error: Content is protected !!