Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Lissu aachiwa kwa dhamana, aenda Arusha
Habari MchanganyikoTangulizi

Lissu aachiwa kwa dhamana, aenda Arusha

Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki
Spread the love

TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki ameachiwa kwa dhamana ya Sh. 10 milioni na moja kwa moja anaenda Arusha kwenye uchaguzi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), anaandika Faki Sosi.

Lissu alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo asubuhi mbele ya Respecios Mwijage,  Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo,baada ya kukamtwa jana mjini Dodoma na kuletwa Dar es Salaam kwa mahojiano na kufikishwa mahakamani.

Faraja Nchimbi wakili Mwandamizi wa Serikali amedai kuwa Lissu anatuhumiwa kwa kutoa maneno yenye uchochezi ambayo yangeweza kupelekea uhasama ndani ya jamii kupitia imani ya dini.

Lissu ambaye amejitetea mwenyewe amekana mashtaka yote na upande wa mashtaka umedai upelelezi umekamilika na wameomba wamsomee maelezo ya awali leo, lakini mshtakiwa aliomba maelezo hayo ya awali yasomwe Jumatatu, ili aweze kuhudhuria uchaguzi wa TLS unaotarajia kufanyika kesho.

Baada ya Lissu kuachiwa kwa dhamana aliwaambia waandishi wa habari kuwa baada ya kuwa huru anaelekea jijini Arsuha kushiriki uchaguzi wa TLS ambao yeye ni mmoja wa wagombea katika uchaguzi huo.

Lissu ni kati ya wagombea wa watano wanaowania nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho, lakini amekuwa akikumbana na changamoto kadhaa ikiwemo kufunguliwa kesi mbili za kupinga uchaguzi huo, lakini zote zimetupiliwa mbali, hivyo uchaguzi utaendelea.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika kesho Machi 18, 2017 jijini Arusha na maandalizi yote yamekamilika.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!