January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

9 wajitosa CCM kumrithi Ndugai

Spread the love

 

WANACHAMA tisa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania wamejitosa kuchukua fomu kuwania uspika wa Bunge la nchi hiyo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Fomu hizo zimeanza kutolea leo Jumatatu, tarehe 10-15 Januari 2022, katika Ofisi ndogo za Lumumba jijini Dar es Salaam, Kisiwandui, Zanzibar pamoja na Makao Makuu ya chama hicho, jijini Dodoma.

CCM inaendesha mchakato wa kumpata mgombea uspika, baada ya aliyekuwa spika wa Bunge, Job Ndugai kujiuzulu nafasi yake tarehe 6 Januari 2022, kutokana na kauli yake aliyoitoa kuhusu serikali kukopa kuibua mjadala mkali.

Akitoa taarifa ya uchukuaji fomu, katibu msaidizi mkuu idara ya oganaizesheni, Salomon Itunda amesema, waliochukulia ofisi ya Dodoma ni sita na Lumumba jijini Dar es Salaam wakiwa watatu.

Kati ya wanachama hao tisa waliojitosa kuchukua fomu yumo, Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson pamoja na Mbunge wa Mlimba mkoani Morogoro, Godwin Kunambi waliochukua fomu zao jijini Dodoma.

Wengine waliochukua Dodoma ni, Dk. Saimon Ngatunga, Tumsifu Mwansamale,
Merkion Ndofu na Ambwene Kajula.

Waliochukulia ofisi ya Lumumba ni, Patrick Nkandi, Hamidu Chamani na Stephen Massele ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Shinyanga Mjini na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP).

error: Content is protected !!