January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watoto 2 wafariki dunia ndani ya gari Dar

Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam

Spread the love

 

WATOTO wawili wamefariki dunia jana Jumapili, tarehe 9 Januari 2022, baada ya kujifungia ndani ya gari huku wakiwa wamefunga vioo na kukosa hewa, Mtaa wa Salanga, Kigamboni jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema, tukio hilo lilitokea mchana wa jana Jumapili, wakati mama yao, Neema Shayo (33), akiwa katika Ibada Kanisa la Efatha, Ungindoni Kigamboni.

Amesema, mama huyo alimwagiza binti wa kazi, Odilia Msamba (18) kwenda kumpa dawa Abia Joseph (2) ambazo zilikuwa katika gari namba T 850 DWL aina ya Nissan Double Keben iliyokuwa nje ya kanisa.

Amesema watoto hao watoto hao waliamua kulala ndani ya gari hilo wakiwa wamefunga vioo na baada ya muda mrefu kupita, mama huyo alikwenda kuwaangalia na kuwakuta kwenye hali mbaya na kuwapeleka hospitalini haraka lakini baadaye ilibainika wamefariki dunia.

Kamanda Muliro amewataka wazazi na walezi kuchukua tahadhari hasa wanaposhughulika au kuwatuma mabinti wanaowasaidia kazi ambao hawajui uwezo na maarifa waliyonayo juu ya mambo wanayowatuma.

error: Content is protected !!